Tetesi za soka na usajiri
Bayern Munich wanatarajiwa kutoa ofa nzuri zaidi yenye thamani ya karibu pauni milioni 70 kwa ajili ya mshambuliaji wa England Harry Kane lakini ofa hiyo haiwezi kufikia thamani ya Tottenham, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kusalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake. (Chanzo: Mail on Sunday)
Chelsea wanataka pauni milioni 40 kwa anayetaka kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, ambaye anavivutia vilabu vya Al-Hilal na Juventus, wakati Inter Milan wamekataliwa ofa yao waliyotoa awali kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Chanzo: Guardian)
Manchester United wamekubaliana masharti binafsi na mshambuliaji wa Denmark, Rasmus Hojlund na yuko tayari kuiomba Atalanta kumruhusu kuondoka ikiwa klabu hiyo ya Old Trafford haiwezi kuafikiana na klabu hiyo ya Italia, ambayo inataka £60m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Chanzo: Football transfers)
Tottenham wanamfuatilia Mhispania wa Chelsea Marc Cucurella, 24, ambaye anaweza kucheza kama beki wa kushoto au winga wa upande wa kushoto, huku wakati huu wakitafuta mbadala wa winga wao wa Croatia Ivan Perisic, 34. (Chanzo: Football Transfers).
FOLLOW US HERE