Mbaroni kwa kumbaka mwanamke mwenye ujauzito wa miezi 9

 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limemtia mbaroni Muuguzi Rayson Duwe ambaye ni Muuguzi Msaidizi katik Hospitali ya Wilaya ya Sikonge, kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mwenye ujauzito wa miezi tisa, baada ya kumchoma sindano yenye dawa ya usingizi.


Haya yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao wakati akitoa taarifa ya tukio hilo ambalo amelitaja kuwa sio la kiungwana na kwamba limetokea June 9, mwaka huu saa mbili usiku ambapo mwanamake huyo alikuwa akipata matibabu ya malaria hospitalini hapo.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, inadaiwa kuwa muuguzi huyo ambaye aliingia kazini akiwa amelewa, alitenda kosa hilo wakati alipopangiwa zamu ya usiku ya kuhudumia wagonjwa wa nje, ambapo alitoka na kwenda chumba cha wagonjwa wa ndani na kumbaka mama huyo mwenye ujauzito wa karibu kujifungua.

Muuguzi huyo alikutwa akiwa na bomba la sindano pamoja na dawa za usingizi huku taarifa ya kitabibu zikithibitisha kuwa alimwingilia mgonjwa huyo.

Mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakani mapema hii leo June 13, 2023 kujibu tuhuma zinazo mkabili baada ya upelelezi kukamilika.