Raisi Samia afanya uteuzi washauri wa Raisi


Taarifa kutoka Idara ya mawasiliano ya Ikulu imeripoti;

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi Washauri wa Rais wafuatao:-

(i) Amemteua Mhe. William Vangimembe Lukuvi (Mb.) kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Mhe. Lukuvi ni Mbunge wa Jimbo la Ismani, Iringa;

(ii) Amemteua Bw. Abdallah Bulembo kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bw. Bulembo ni Mbunge Mstaafu;

(iti) Amemteua Balozi Rajab Omar Luhwavi kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Balozi Luhwavi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji; na

(iv) Amemteua Bw. Haji Omar Kheir kuwa Mshauri wa Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii). Bw. Kheir ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Waziri Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Uteuzi huu umeanza tarehe 13 Juni, 2023.