SIMULIZI: BODABODA WA MKE WANGU

Kulikuwa na kijana mmoja aliitwa Prince, alikuwa ni bodaboda aliyekuwa jirani yetu, tulikuwa tunamwamini na hata kumpa baadhi ya mizigo yetu ya msingi atupelekee mahali tulipotaka ifike





Huu ni utaratibu wa kawaida kwa familia zetu za mjini. Kwa sababu tulimuamini, mke wangu alikuwa akimtumia sana katika safari zake, mimi kiuhalisia sikuwa nikimtumia maana mm sio mtu wa kukaa nyumbani, niko bize na kazi zangu, nilimtumia tu pale ambapo labda niko nyumbani na nahitaji kufikisha mzigo fulani mahali na mke wangu ndiye aliyekuwa aki-suggest kuwa tumpigie Prince apeleke, ndo maana mimi nilikuwa nikimuona kama bodaboda wa mke wangu.

Basi mke wangu yeye katika safari zake zote kila alipotaka kwenda, ni kumpigia prince aje ampelekee.


Karibia safari zote za mke wangu Prince alikuwa akizijua, na mimi binafsi sikuwa na wasiwasi na prince kwa sababu hiyo ni biashara kama biashara nyingine na mtu hufanya biashara na anayemuamini.

Hata baada ya kuja hizi Bolt na Ubber ambazo mtu aki-request gharama zinakuwa chini kuliko gharama za bodaboda wa kawaida, lakini bado mke wangu yeye aliendelea kumtumia Prince kwenye safari zake ijapokuwa nilimshauri hilo, pia haikuwa shida kwangu maana niliona sio mbaya as long as prince ni mtu tunamuamini


Sasa ikafika hatua prince akawa family friend, akawa anakuja nyumbani kama siku za mechi hivii, anakuja kuangalia mechi za Ulaya tunafurahi maisha yanaendelea na mambo mengine madogo madogo tunapiga tu story kawaida.


Basi ilitokea hiyo siku moja nimesafiri nimeenda mkoani,

Nipo huko usiku mida ya saa nne hivi, nilikuwa hotelini ambapo nilikuwa nimefikia na ilikuwa ni safari ya kikazi,

Basi nikapokea simu kutoka kwa dada mfanyakazi wa pale nyumbani, akaniambia “kaka kuna vurugu hapa ndani, Prince anagombana na dada (mke wangu)” nikawa namuuliza “shida ni nini?!”

Alikata simu maana hata kunipigia alikuwa anaongea kiuogauoga.

Napiga tena akawa hapokei

Niliwaza ni nini kinachoendelea huko nikawa sielewi. Ugomvi wa mke wangu na Prince umeanzia wapi? Na Prince anatafuta nini hapo nyumbani usiku wote huo?!

Niliwaza sana nafanya nini nikawa sielewi.

Nilimpigia mke wangu na yeye akawa hapokei simu kabisaa, nikampigia huyo huyo Prince na yeye akawa hapokei simu.

Niliwaza sanaaa, lakini sipati majibu nifanyeje


Nilimpigia rafiki yangu Amoni anisaidie kufika nyumbani aangalie kuna nini kinachoendelea.

Amoni mara ya kwanza hakupokea, nikaelewa ni kwa sababu ni usiku sana, yawezekana amelala.

Baadaye nikampigia tena, akapokea namuuliza kama yupo kwake ananiambia yupo club, halafu sasa hiyo club ni mbali na nyumbani, nikamwambia atoke nje sehemu iliyotulia tuongee mara moja.

Akasema sawa


Nasubiria atoke nje anipigie jamaa hapigi, nikasubiria sanaa Ikabidi nimpigie tena, hapokei, nampigia mara ya pili ndo akapokea akaniambia anatoka nisubirie mara moja Basi ndo akawa ametoka akanipigia, kumbe ameshalewa hadi kulewa ndo sababu ya usumbufu wote


Nikamuuliza “kwani uko na nani”akanitajia washkaji wengine aliokuwa nao nikamwambia anipe fulani niongee naye, akaingia ndani na kumcheki akamtoa nje ndo nikaongea naye, bahati nzuri yeye alikuwa hajalewa na nililijua hilo ndo maana nikamwambia nipe fulani, basi huyo jamaa nikamueleza kinachoendelea, nikamuomba anisaidie kufika nyumbani haraka kuangalia usalama maana hapa nimeshajaribu kila namna, Nimecheki hadi jirani yangu mmoja hivii naona ameshalala


Jamaa akasema sawa sawa ngoja tuelekee huko, Alimchukua Amoni na pombe zake wakaenda nyumbani kwangu njiani akawa anamueleza Amoni kinachoendelea, Sasa walienda wakafika kwangu wakakuta kuko kimya, watu wote wamelala. Ikabidi wagonge mlango


Waligonga na kugonga lakini wapi, hakuna mtu anafungua mlango


Wakajaribu kuita lakini wapi kuko kimya, sasa wasiwasi wao ukawa ni hawaelewi kuna watu humo ndani au hakuna mtu, walimuita sana mke wangu lakini hakuna anayeitika humo ndani, waliogopa hata kunieleza kinachoendelea


ila ilibidi tu wanipigie na kuniambia kuwa waligonga mpaka kidogo wavunje mlango lakini hakuna hata mmoja anayejitingisha.


Sasa hawaelewi kuna nini kinachoendelea


Niliwaambia, sasa fanyeni hivii, muibukieni Prince. Nendeni kwake, mfikieni mjue nini kinachoendelea Walienda kwa Prince walifika kwake wakagonga mlango ukafunguliwa, unafunguliwa anatoka rafiki yake Prince


Wakamuuliza prince yuko wapi, Akawajibu Prince tangu alipoondoka hapa saa mbili hajarudi mpaka saivi, Wakamuuliza kama hakuna mahali anahisi atakuwepo, akasema hapana, maana yule ni bodaboda naweza kuwa mahali popote kulingana na wateja wake

Wakamwambia basi fanya hivii, mpigie simu Jamaa akampigia simu Prince, simu ikaita lakini haipokelewi.

Akapiga tena haipokelewi,

Alipopiga mara ya tatu simu ikawa haipatikani, ikiwa na maana Prince amezima simu 

Walichokaa, wakanipigia simu kunielezea yote hayo ambayo yametokea, nilichoka piaa

Wakati huo mke wangu naye simu haipatikani tena, dada wa kazi yeye hapokei


Nini kinachoendelea hapaaa?

Mke wangu na dada wa kazi wako wapi?! Zile zilikuwa ni vurugu za nini?!

Prince na yeye kaenda wapi?!

Maswali yote haya nilijiuliza bila kuwa na majibu yake, marafiki zangu waliniomba niwaruhusu wakapumzike kwanza, kesho asubuhi na mapema wataamka na hilo. Ilikuwa ngumu kuwaruhusu waende kwao kupumzika, lakini hata nikiwakatalia, wabaki waendelee kufanya nini maana huo ulikuwa ni usiku wa saa saba tayari


Unaweza sasa kupata break fupi kwa ajili ya sehemu ya pili ya story hii



SEHEMU YA PILI


Asubuhi na mapema nampigia Amoni rafiki yangu namwambia aende nyumbani kwangu haraka, kama alivyoniahidi kuwa nimruhusu apumzike na asubuhi na mapema wataamkia kwangu kuangalia usalama.

Alienda peke yake nyumbani kwangu


Alienda na kufika nyumbani kwangu alimkuta mke wangu yupo pale nyumbani, akaongea naye kuhusu ilivyokuwa jana na jinsi ambavyo waligonga mlango hakuna aliyefungua wala anayejitingisha humo ndani, akamuuliza kuna usalama wowote na nini kinachoendelea?!


Sasa kabla hajafika na kumuuliza, mimi nilikuwa nimeshampigia tena mke wangu kabla. Yaani baada ya kumpigia Amoni akaenda nyumbani kuona usalama ukoje, nilimpigia tena mke wangu ambaye tangu jana alikuwa hapatikani baada ya kumpigia mara ya kwanza asipokee, safari hii akapokea


nilishtuka kuona kapokea, atleast naweza kujua kinachoendelea.

Nikamuuliza kuna nini huko mbona tangu jana sikupati na wala simu yangu hupokei?

Akaniambia jana alichoka sanaa hivyo alilala mapema sanaa na simu yake haikuwa na chaji hivyo ilikaa on na baada ya muda ikajizima kwa chaji kuisha.

Sasa binafsi mwanzo sikuwaza kama kunaweza kuwa na kitu cha yeye kunificha, nilikuwa nikimuamini sanaa, na hata hili la kutokumuambia kuwa nilipigiwa na dada wa kazi akaniambia kuna vurugu huku sio kwamba nilikuwa nimepanga kumficha, ila nilianza tu taratibu kuwa mbona jana ulikuwa hupokei simu na baadaye kutokupatikana ili anielezee yeye mwenyewe tatizo, maana mimi nilichokifikiria ni kutakuwa na tatizo, japo niliwaza sana bila kupata majibu kuwa ni matatizo gani huyo jamaa anaweza kuyaleta hapo nyumbani maana ni mtu tunayemuamini vizuri tu.


Basi aliponiambia vile halafu akawa hajanieleza chochote, ilibidi ninyamaze kwanza nisimuelezee kuwa dada wa kazi alinipigia halafu akawa hajanielezea vizuri akakata simu.

Nilimwambia sawa haina shida, tukazungumza mazungumzo mengine, ila sikuwa sawa hata kidogo 

moyoni mwangu nikawa nikijiuliza ni kitu gani huyu mke wangu ananificha hapaa.


Na sasa rafiki yangu Amoni anafika kwangu na kuanza kumuelezea mke wangu kilichotokea jana, anataka afahamu shida ni nini ili akanieleze.

Mke wangu alishtushwa sanaa na kile ambacho alikiskia kutoka kwa Amoni, akakumbuka jinsi alivyonidanganya kwenye simu kuwa hakuna shida yoyote ni simu tu haikuwa na chaji na yeye alikuwa ameshalala.

Sasa huo mshtuko Amoni ndiye aliyeuona vizuri na kunisimulia kuwa mke wako baada ya kumuelezea kuhusu kilichotuleta jana usiku na akashindwa kufungua mlango, ameonekana kushtuka mnoo ndo mimi nikaelewa sababu ya kushtuka kwake ambayo ni kama nilivyowaeleza.

Mke wangu alimwambia Amoni kuwa yeye alikuwa amelala na alikuwa na usingizi sana, sauti aliziskia lakini hakujua ni za akina nani hivyo hakutaka kufungua kabisaa hivyo ikabidi akae kimya.


Sasa Amoni akamuuliza kwani dada huyu (dada wa kazi) hakutufahamu kuwa ni sisi akafungua au na yeye alikuwa anausingizi kama wewe? Alimjibu kuwa, alishagamzuia kufungua mlango kwa mgeni yoyote usiku wakiwa wameshalala tayari.

Basi, akamwambia kuwa usalama upo wala asiwe na wasiwasi, na kuhusiana na suala hilo la vurugu za yeye na Prince (yule Dereva bodaboda) asijali yeye ataongea na mume wake ila sio issue kubwa.

Na hivyo ndivyo alivyonieleza Amoni baada ya kutoka kwa mke wangu


Sasa Amoni pamoja na na kunielezea yote hayo ila ilibidi pia anielezee mtazamo wake binafsi,

Aliniambia mke wangu kwanza alishtuka nilivyoelezea kilichotuleza nyumbani usiku huo tukigonga na asifungue, jambo ambalo linatia wasiwasi, lakini pia anadanganya kusema alikuwa na usingizi na kuwa hakujua sisi ni akina nani, kwa sababu mlango tuliugonga kwa nguvu zote lakini hakuna mtu anaitikia, na kwa sababu tulikuwa na wasiwasi kuwa kunaweza kuwa na shida ndani kama ulivyotueleza, tulitaka hadi kuuvunja huo mlango ndo baadaye tukaona tuache kwanza tukusikilize, ndo ukatuambia twende kwa prince mwenyewe. Huyo mtu anausingizi gani huo? Hata Samaki hawalali hivo. Lakini pia anasema hakujua sisi ni akina nani, hiyo ni uongo kwa sababu tulikuwa tunaita kabisaa “shemeji, ni mimi Amoni” fungua mlango, fungua, kuna usalama huko?”


kiufupi majina yetu tuliyataja hata kama alikuwa hajui sauti kwa sababu ya usingizi basi hata majina yetu angeyaskia.

Akaniambia, mchunguze mke wako, kaka nahisi umepigwaa 


Nilichokaa, na muda huo nilipaswa niwe kwenye kikao kwa ajili ya mambo ya kikazi hayo yaliyonipeleka mkoani


Nilichelewa kikao kwa muda mrefu kweli, na pia hata baada ya kuingia, akili yangu haikuwa sawa, nikiwaza mke wangu ana kitu gani ananificha.

Kila nikijaribu kuwaza may be kuna cheating ananifanyia kwa huyo bodaboda, naishiwa nguvu, najilazimisha kukataa kuwa haiwezekani Kabisaa


Nilimaliza hicho kikao kwa mbinde na nilirudi hotelini nikiwaza nifanye nini, simu za mke wangu zikawa zinaingia sipokei maana nina hasira sana, kwanini anidanganye au kunificha kitu mimi mume wake, au ananicheat hapaa


Niliwaza sanaa na ndipo nilipoamua kumpigia tena dada wa kazi.

Dada alipokea nikaongea naye kitaratibu ili asiogope aweze kunielezea.

Nilimuuliza jana hizo vurugu ulizokuwa unazisema hapo nyumbani uliponipigia ni zipi? Kuna nini kinaendelea?!

Nieleze wala usiogope


Akaogopa kabisa kusema, akaniambia kaka mimi naogopa nikiongea chochote dada atanitoa roho mimi naomba tu wewe mwenyewe umpigie umuulize, ni mke wako yule, akuelezee au wewe mwenyewe fuatilia tu mwenyewe kujua kinachoendelea,

Maana mimi hapa hata sina amani, dada amejua kuwa nilikupigia simu kukwambia kuna vurugu ndani za yeye na Prince amenigombeza tangu asubuhi ni kunisema na amesema nitarudi nyumbani kwa sababu ya huu mdomo wangu, amenipiga na kunipiga, amenikasirikia sanaa hataki hata kuniona. Naogopa sana na yeye ndo alinileta hapa kufanya kazi


Ilinibidi nikate simu.

Nikajikaza kiume kuhudhuria kikao cha kesho yake ambacho kilikuwa ni cha mwisho

Ambacho kiliisha jioni kabisaa, na hivyo kesho yake asubuhi na mapema nikaanza safari ya kurudi nyumbani, nikiwa na hasara nyingi mnooo


Mpenzi msomaji, unaweza kupata mapunziko kidogo sanaa kwa ajili ya kumalizia sehemu ya mwisho ambayo ukweli unaenda kugundulika na utajua ni nini hasa kilichokuwa kinaendelea



SEHEMU YA TATU 

(The Last Episode)


Kutokana na ukaribu wa mara kwa mara ambao mke wangu alikuwa nao na huyo Dereva wake wa bodaboda, zilianza kujengeka hisia katikati yao, zilianza kama utani, wakitaniana mambo ya kimapenzi lakini sasa ikafika hatua hisia zao zikawa more serious, marafiki zake Prince (huyo dereva wa bodaboda) walikuwa kila siku ni kumcheka jinsi ambavyo mtoto anaonekana kumuelewa lakini yeye anakuwa muoga. Bodaboda wenzake walimuona zuzu sana kwa sababu amekuwa na ukaribu mnoo na mke wangu mpaka wote wanaonyeshana hisia za kupendana lakini yeye anakuwa muoga kisa mimi mume wake huyo mwanamke, walimwambia unapaswa kuhit and run, huyo ni mke wa mtu lakini anajilengesha kwako kila siku halafu wewe umezubaa.

kibaya zaidi ni kuwa huyo mke wangu alikuwa ni mzuri sanaaa, sasa na hiyo marafiki zake wakasimama nayo kama point kumshangaa huyo Prince anavumilia vipi, na Wakamwambia hizo chance ni mara moja kwa life time, huwezi pata tena, japo pia wapo wengine ambao walimuonya asiwasikilize hao.

Kitu nilichojifunza hapa ni kuwa, hakuna jambo baya kama mke wa mtu kuruhusu mazoea na mwanaume mwingine, hilo jambo ni hatarii mnoo japo sio mara zote litakuwa hatari, maana mke wangu na Prince walianza na uteja kama kawaida, yaani mke wangu alikuwa mteja mzuri wa Prince, safari zake anamuita Prince ampeleke, lakini ile kuwa na free time mara kwa mara, akitaka kwenda huku yuko naye kule yuko naye, hakuna bodaboda yeyote tofauti anayemtumia mpaka sasa ikafika hatua jamaa akawa family friend anaweza kuja nyumbani muda wowote na akaondoka muda wowote, binafsi mm hata mara moja sikuwahi kuhisi kama kuna kitu kitakuja kutokea, nilikuwa nikimuamini sana Prince na mke wangu nilimuamini pia. Kumbe mazoea yao yalikuja kuzaa mapenzi. Maana sasa prince aliona anachoshauriwa na marafiki zake ni kweli, na kwanza isitoshe yeye mwenyewe kwa muda mrefu sana amekuwa akitamani ni vile tu aliniogopa mimi


Yote hayo nilisimuliwa na rafiki yangu Amoni ile siku nimekuja kutoka safarini huko mkoani.

Wakati nipo njiani nilimpigia na kumueleza kila kitu kuhusu mazungumzo yangu na yule dada wa kazi, nikamwambia jinsi ambavyo nimegundua mke wangu kuna kitu kikubwa sanaa ananificha

Nina hasira sanaa na ninaenda kujua ni kitu gani hicho japo ninasuspect cheating hapo. Na kwa kweli moyo unaniuma mnoo, mke wangu nilimuamini sanaa. Amoni akaniambia, kabla hujafika kwako njoo upitie kwanza kwangu kuna file la mke wako ninalo.

Nilishtuka sanaa, nikamuuliza file gani? Akaniambia straight, file la mke wako na huyo Prince.

Nilihisi kuchanganyikiwa yaani, niliendesha gari kama kichaa, mpaka ikanipelekea kusumbuana na traffic police huko njiani, lakini ni kwa sababu stress zilikuwa ni nyingi kichwani.


Nilifika kwa Amoni, Akaanza kunieleza Kuwa baada ya kuondoka kuongea na mke wangu na akaona jinsi ambavyo kuna kitu mke wangu anaficha (kama tulivyoona sehemu iliyopita) plus na zile doubt alizokuwa nazo

Aliwaza, akaamua kumtafuta mshikaji wake ambaye alikuwa ni bodaboda wa kile kile kituo cha Prince, lakini pia na yeye alikuwa na ukaribu na Prince, alimpigia simu akamuomba wakutane, ile wamekutana kwanza akampiga castle lite tatu, jamaa alikuwa ni mpenzi sanaa wa castle lite

Halafu ndo akamuuliza sasa anafahamu vipi kuhusu Prince na mke wangu 

Inshort alimtengenezea mazingira mazuri ya yeye kuropoka kila kitu. Ndo jamaa akamsimulia kila kitu kama nilivyozungumza hapo awali, kumbe jamaa alikuwa anawasimulia yote yanayoendelea ili kuwaonyesha yeye sio mnyonge.

Na kumbe hata ule usiku wamekuja kugonga nje mlangoni, Prince alikuwepo ndani.


Sasa ndugu msomaji, 

kuhusu zile vurugu zilikuwa zinahusu nini ambazo hadi dada alinipigia simu, hilo nitakuachia mwenyewe kutafsiri. 

Ila ukweli ni kuwa usiku huo Prince alilala humo ndani na asubuhi na mapema akarudi kwake, akaenda kuwasimulia washikaji zake baadaye pale kijiweni


Baada ya rafiki yangu Amoni kunisimulia hayo yote. Jasho lilikuwa likinitoka na imagine sipati picha, Speed ya kwanza nilifikia kwa Prince kabla ya kwenda kwangu baada ya kutoka kwa Amoni.

Nilifika nikaambiwa Prince amehama, jana usiku kaondoka na vitu vyake.


Kumbe mke wangu alipomueleza kuwa nimejua aliona hiki ni kifo, alihama usiku huo, sijui alihamia wapi kwa haraka kiasi hicho.

Nilijaribu kuwauliza kama wanafahamu alikohamia majirani wote hakuna anayefahamu.

Ndipo Amoni akaniambia, huyo hajahamia sehemu bado ila atakuwa kwa washikaji zake, issue ni kujua yupo kwa nani. Ilibidi tuachane naye nikadeal na mke wangu anieleze vizuri hili.

Nilienda mpaka nyumbani namkuta dada wa kazi peke yake, mke wangu hayupo.

Akaniambia dada ameondoka,

Sijui kaenda wapi, ila hakuwa sawa kabisaa Na amekataa  Kuniambia anapoenda

Wazo lililoniijia haraka haraka ni kuwa ametoroka na Prince.

Hakya Mungu nilitamani njiripue.

Nilienda kwa kila niliyemjua ni mtu wa karibu wa Prince anieleze Prince yuko wapi na mke wangu lakini wote hakuna aliyenipa jibu la Prince alipo, japo nina uhakika Katika wote wale niliowapitia yupo mmoja ambaye alikuwa akijua Prince alipo, ni vile tu huwezi jua ni nani.

Niliamua kupiga simu nyumbani kwao mke wangu, wakasema hayupo huko, ikabidi niwaeleze kwa ufupi kinachoendelea, na wao wakaanza kuhaha huko, nikajua kabisaa huyu kaenda na Prince kweli, kama hata kwao hawajui alipo. Baadaye kidogo nikapokea simu ya dada yangu ananiambia mke wangu yupo kwake analia tangu amekuja, ananiomba mimi msamaha na anasema nimtafute mume wake,

Ikabidi niende kwa dada nimeenda nikamkuta kumbe yupo huko, na kumbe kashamueleza dada kila kitu, akikiri makosa yake na kuomba msamaha

Nikamueleza dada aibu hii yeye angekuwa ndio mimi angeivumilia vipi?!

Nikamwambia dada, hii aibu mimi siwezi ivumilia na huu ukatili niliotendewa na huyu mwanamke ni kama mauti.


Wakati tunaendelea kuongea, ndugu zake mke wangu walinitafuta kujua nimefikia wapi kumpata mtoto wao, na walinipigia wakiwa kwangu kumbe na wao walikuwa wanahangaika kumtafuta tangu pale nilipowapigia kuwaeleza kupotea kwa mke wangu.

Nikawaambia njooni huku kwa dada ndio yupo huku, niliwaelekeza kwa dada ni wapi wakafika


Niliwaambia kila kitu from A to Z. Hadi wao walijiskia aibu sana kwa kile alichokifanya mtoto wao, wakamuombea msamaha maana alikuwa akilia tangu wamekuja anaomba tu msamaha.

Mimi niliwaambia ni ngumu kuuforce moyo ambao umevunjika namna hii eti uanze kumpenda mtu tena, naomba Mchukueni mwende naye, siku nikiwa tayari kurudiana naye nitakuja kumchukua.

Na hiyo ndo ilikuwa my final say baada ya mazungumzo yote.

Waliondoka naye, hakutaka kuchukua kitu chochote nyumbani aliondoka hivo hivo, akisubiria hasira zangu ziishe.


Mpaka sasa bado nasubiria moyo Wangu ukiwa tayari kuwa naye, ndipo nitaenda kumchukua.

Ila kwa alichonitendea, itachukua muda mrefu sana kumsamehe arudi nyumbani.


Eeh bhana sina la ziada. Mwisho wa story yetu.


Ni mimi Mtunzi na Mwandishi wako

Damas Bayona


Unaweza kutupata sehemu hizi hapa pia 👇👇


Whatsap: https://wa.me/255747671795

Twitter: https://twitter.com/bayona_stories

Instagram: https://www.instagram.com/bayona_stories/

Tiktok: https://www.tiktok.com/@bayona_stories

YouTube: https://www.youtube.com/@Bayona_stories