Singida Big Stars sasa kuitwa Singida Fountain Gate FC

 


Baada ya kupata mmiliki mpya Club ya Singida Big Stars imebadilisha jina na itakuwa ikiitwa Singida Fountain Gate FC. Hii ni kutokana na mmiliki mpya wa Club hiyo Japhet Makau kuwa mmiliki wa shule za Fountain gate na pia ni mmliki wa timu ya Fountain Gate FC inayoshiriki championship na timu ya wanawake ya Fountain gate princess.

Ikumbukwe pia kuwa singida big stars ni mmoja wa wawakilishi katika mshindano ya kimataifa katika msimu ujao akiungana na Simba sc, Yanga sc na Azam FC