Brazil kuvaa jezi nyeusi mechi yao ya kwanza kuonyesha kampeni yao dhidi ya ubaguzi wa Rangi


 Katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Guinea, Timu ya Brazil wamevaa jezi nyeusi kuonyesha kampeni yao ya kupinga ubaguzi wa rangi

Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita wakati wa kumalizia ligi kule nchini Hispania (La Liga), mchezaji wa Real Madrid ambaye ni mwanasoka wa Brazil Vinicius Jr, alionyeshwa vitendo vya ubaguzi wa rangi wakati timu yake ikicheza dhidi ya Valencia katika kuhitimisha mbio za msimu huo wa 2022/2023

Jambo hilo lilizua hisia za wengi hasa pale ambapo maamuzi ya Refa uwanjani yalipokuja kuwa, Vinicius Jr kupewa kadi nyekundu baada ya mabishano yake na wachezaji hao wa timu ya Valencia pamoja na mashabiki wa Valencia ambao walimuonyesha vitendo vya ubaguzi pale uwanjani

Baada ya tukio lile Vin Jr aliituhumu sana La Liga kwa kushindwa kudhibiti/kushughulikia vitendo hivyo vya ubaguzi wa rangi ambavyo vimekuwa vikitokea mara nyingi katika ligi hiyo bila hatua zozote.

Hisia za mashabiki na wachezaji wengi wa soka ziliibuka na mengi yalipigiwa kelele kwa la liga na kwa watu hao walioonyesha vitendo vya ubaguzi wa rangi

Hata hivyo La Liga haikuweza kuchukua hatua zozote dhidi ya timu ambayo hao wahusika walikuwa zaidi ya kuripoti hao wahusika kwa serikali ya nchi hiyo. Kwani sheria za nchi hiyo zinainyima mamlaka La Liga kufanya maamuzi yoyote kwa timu inayoonyesha vitendo vya namna hiyo kwa mchezaji au mtu yeyote 

Jambo hilo lilionekana kutokuwa sawa kwani linachochea na halidhibiti vitendo hivyo vya ubaguzi wa rangi.

Vinicius Jr aliahidi kutokuondoka Real Madrid au nje ya La Liga kwa sababu ya vitendo hivyo bali ataendeleza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi akiwa kulekule