Haaland alifunga bao la kwanza katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Scotland mjini Oslo, akifunga penalti dakika ya 61, lakini alitolewa kwa dakika ya 84 na bao 1-0.
Mabao mawili ya dakika za lala salama yamewapa wageni ushindi wa kushangaza wa 2-1, Lyndon Dykes alifunga dakika ya 87, na Kenny McLean akafunga la ushindi dakika mbili baadaye.
Mshindi huyo wa mataji matatu ya Manchester City ameondoka uwanjani akiwa hajafurahishwa na kilichotokea, akenda moja kwa moja kwa kocha na kuwavunja moyo mashabiki waliokuwa wakimgoja akasaini kwenye vibao vyao, kwa kususia kuandika popote, ambapo wameonyesha kutofurahishwa kwao na kuanza kumzomea
Haaland na Norway sasa zinakabiliwa na kibarua kikubwa cha kufuzu kwa Euro 2024 kwani zimeshindwa kushinda mechi yoyote kati ya tatu za kwanza za kufuzu, pia kupoteza kwa Uhispania na kutoka sare na Georgia.
Scotland sasa, wako kileleni mwa kundi hilo wakiwa na alama tisa
Norway itacheza na Cyprus siku ya Jumanne inapojaribu kuendeleza kampeni ya kufuzu na kupata ushindi wao wa kwanza.
Chanzo: goal.com
FOLLOW US HERE