HESLB: Maombi ya mkopo kwa ajili ya elimu ya juu kuanza July 15 mwaka huu

 


Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu Tanzania HESLB jana tarehe 08 wametangaza siku maalumu ya kuanza kupokea maombi ya mikopo kwa ajili ya elimu ya juu kuwa itakuwa ni kuanzia July 15

Hiyo ni kutokana na kuwa HESLB inafanya mabadiliko ya mfumo mpya utakaoanza kutumika 2023/2024 ambapo waombaji hawatahitaji kutumia Nakala ngumu (Hard copy) katika uombaji, jambo ambalo litapunguza gharama katika mchakato huo 

HESLB imetangaza kutoa mwongozo wa utoaji mkopo na ruzuku mapema kabla zoezi hilo la kupeleka maombi halijaanza. Waombaji wato wanashauriwa kuupitia na kuuzingatia 

Na muongozo huo utapatikana katika tovuti ya bodi hiyo