DC avunja ndoa ya mwanafunzi iliyotolewa kwa mahali ya 30,000

 


Mkuu wa wilaya ya Tunduru ameivunja ndoa ya binti mwanafunzi ambaye anategemewa kujiunga na kidato cha tano Agosti mwaka huu 

Ndoa hiyo iliyofungwa kwa mahari ya Tshs 30,000 ameivunja leo mkuu wa wilaya hiyo na mwanafunzi huyo kupaswa kuendelea na kidato cha tano kwani alikiri kuwa tayari kama atapata nafasi hiyo ilihali wakati huo huo baba yake alisema kuwa ni yeye alitaka kuolewa na sio kuendelea na masomo na kupelekea kutishia kuwa kama ataendelea kulazimishwa kwenda shule atabeba mimba kwa makusudi ili asiende

Mkuu wa wilaya hiyo amewaasa wananchi kuacha tamaduni hizo potofu na kuwapa watoto haki yao ya elimu