Alikuwepo mzee mmoja ambaye alikuwa na miaka mingi sana katika kazi yake aliyokuwa akiifanya. Mzee huyo hata ulipofika umri wa kustaafu bado aliombwa aendelee kufanya kazi hata kama itakuwa sio sana. Ila aliombwa aendelee maana alikuwa na uzoefu kuliko mtu yeyote yule katika kazi ile na aliaminika sana, na kweli ‘performance’ yake ya kazi ilikuwa ni nzuri sana.
Kulikuwa na kijana mmoja kwa jina la Dauson, alikuwa akitafuta kazi kwa muda mrefu, alihangaika na kuzunguka kila mahali lakini juhudi zake zilikuwa hazifui dafu. Alikuwa na rafiki yake aliyeitwa Onesmo. Na kumbe huyo Onesmo alikuwa ndio mjukuu wa huyo mzee niliyemueleza hapo awali.
Huyo mzee alimpenda sanaa Onesmo kuliko wajukuu zake wote aliokuwa nao.
Na ndiye aliyekuwa akiishi naye. Wajukuu zake wengine wote walikuwa wakiishi kwao, kwa wazazi wao. Ila Onesmo peke yake ndio alikuwa akiishi na babu yake.
Onesmo aliongea na Dauson kuwa babu yake ana ‘bonge moja la kitengo’ huko kazini kwake. Na wanamheshimu sana, hivyo anaweza akafanya jambo kwa ajili yake. “Inabidi baaadaye uandae muda tuongee naye umpange. Akikuelewa, niamini mimi, yule ni bonge la mtu wa kukusaidia kupata kazi pale”
Onesmo yeye alikuwa na kazi tayari siku nyingi tu, hivyo yeye swala la kazi halikuwa tatizo. Walimuomba mzee nafasi ya kuongea naye hilo swala, mzee akamwambia Onesmo, “mwambie tu huyo Dauson aje nimsikilize”
Basi Dauson alienda na kuongea na mzee. Akamuonyesha ni kwa jinsi gani amehangaika kutafuta kazi bila mafanikio na ndio maana sasa yuko tayari kwa kazi yoyote pale ofisini kwake hata kama kwa kuanza mshahara utakuwa ni mdogo.
Mzee alimuuliza maswali yake binafsi ya kumpima na akaona kweli huyu mtu yuko serious na anahitaji msaada. Basi akamwambia kuwa, nafasi za kazi ofisini kwake zimetangazwa kweli, na uhalisia ni kuwa bila kuwa na mtu pale ‘hutoboi’ maana alisema wanahitajika watu watano lakini waliojiandikisha kwa ajili ya ‘interview’ ni watu elfu nne kasoro, unaweza kuona kuwa hapo bila kuwa na mtu humo ndani ni ngumu kupata nafasi.
Akamwambia “ningeongea na mtu ukienda kufanya interview akuweke ila nahisi hata wao saivi wana watu wao, hivyo nalazimika kutumia nguvu niliyonayo kulazimisha niwe katika kikao cha maamuzi ya kuchagua hao watu watano, uzuri ni kuwa kwa ‘structure’ ya uongozi wa kampuni yetu, ninaruhusiwa kuwa kwenye hicho kikao, suala tu ni kuwa sijawahi kuwepo hata mara moja na hii ndo itakuwa mara ya kwanza”
Kwa hiyo mzee akaamua kumsaidia Dauson na akamueleza jinsi atakavyo
msaidia. Mzee alifanya vile kwa sababu ya mapenzi yake kwa mjukuu wake Onesmo, maana Onesmo alimbembeleza sana babu yake amsaidie rafiki yake kwa kila namna, na kwa sababu mzee hakuna kitu cha
thamani kwake kama huyo mjukuu wake, alikubali ku “take any risk”
Basi ilifika siku ambayo kesho yake ndiyo siku ya interview, Dauson akawa anafanya mazoezi mbalimbali ya kujiandaa na interview, maana mzee alikuwa ashamuambia vitu vyote ambavyo wataviuliza na pia vitu ambavyo anatakiwa awe navyo ili kumpa ‘credits’ zaidi
Basi alikuwa bize mitandaoni akitafuta majibu mbalimbali ya maswali hayo na namna ya kuyajibu kwa ufasaha maana ile interview ilikuwa ni Oral interview (yaani unaulizwa kwa mdomo na unajibu kwa mdomo) na nyaraka zote za msingi za kumuongezea ‘credits’ akawa anazitafuta na kuziweka sawa.
Basi siku hiyo hiyo Onesmo alikuja kwake na kumwambia waende swimming pool kuogelea, Dauson akamwambia “si unajua kesho ndo siku ya interview, na mzee juzi amenipa mavitu mengi ya kujiandaa nayo, hapa nipo nakomaa mwanangu” Akamwambia Onesmo, “labda niambie mnaelekea swimming pool ya wapi, ili nikimaliza hizi mambo nije kuungana na ninyi”
Onesmo akamuelekeza swimming pool
wanayoelekea, ambayo ipo katika hotel fulani aliitaja. Sasa akina Onesmo na wenzake wakati wako njiani
kuelekea swimming, wakaamua kubadilisha mawazo, badala waende swimming pool wakaamua waende beach. Wakakubaliana beach ya kwenda, kwa hiyo ‘gear’ ikabadilishwa njiani wakaelekea beach moja hivii, ndio wakaenda kuogelea huko.
Baada ya muda fulani Dauson, akawa amekamilisha mambo yake, akaamua kuwafuata. Sasa yeye aliwafuata swimming pool maana walisahau kumwambia pale walipobadilisha mpango. Hivyo alienda mpaka kwenye hiyo hotel, akafika na akawa hawaoni.
Aliwapigia simu wakawa hawapokei, akajua wameshaanza kuogelea ila akawa hajui ni wapi. Akaona bora arudi zake nyumbani kwao. Lakini wakati yuko njiani, aliamua bora ashukie kituo ambacho ni karibu na kwa kina Onesmo ili walau aonane na yule mzee waongee mawili matatu kwa ajili ya interview ya kesho.
Alifika na kuingia ndani, mlango aliukuta uko wazi. Mara anamuona mzee kaanguka chini, simu yake iko pembeni. Akamuita, lakini mzee haitikii. Akamgeuza, mzee hafanyi chochote. Sasa alipomgusa mshipa wa shingoni ndio akagundua mzee hayuko hai tena. Alijiskia kuweuka.
Haraka haraka akawaza kumpigia Onesmo. Onesmo simu yake, ikawa haipokelewi. Ilimbidi apige simu polisi kwa usalama wake. Maana hajui kilichomuua mzee ni nini, na hakuna mtu yeyote pale ndani.
Polisi walikuja, mwili ukapelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi. Sasa kabla polisi hawajaanza mahojiano naye, mara akapokea simu kutoka kwa rafiki yake aliyeenda na Onesmo, akamwambia , “kaka, Onesmo ametutoka” Dauson akamuuliza, “unaamanisha nini?” akajibu “amefariki”
Hii sasa ndio inaitwa ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni.
Dauson ilibidi agande kama kamwagiwa maji ya baridi, maana huu ulikuwa ni zaidi ya mshtuko kwake.
Nini kimetokea kwa hawa watu wawili, mzee na Onesmo? Kuna jambo gani linaendelea? Vipi kuhusu interview ya kazi?
Inastaajabisha sanaaa hii
Baki na mimi hapa hapa.
Tukutane kwa ajili ya sehemu ya pili
FOLLOW US HERE