WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI 2023.

 


Ofisi ya Raisi TAMISEMI imechapisha katika ukurasa wake wa Twitter 

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI,2023.

Wanafunzi 188,128 waliokidhi vigezo wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na Kidato cha Tano katika shule mbalimbali nchini pamoja na Vyuo vya fani mbalimbali.

(a) Wanafunzi 129,830 wakiwemo wasichana 66,343 na wavulana 63,487 sawa na asilimia 69 ya wenye sifa, wamechaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari za Kidato cha Tano  kwa mchanganuo ufuatao;

(i) Wanafunzi 1,878 wakiwemo wasichana 1,097 na wavulana 781 wamepangiwa katika Shule za sekondari Maalum 8 za Kilakala, Mzumbe, Ilboru, Kisimiri, Msalato, Kibaha, Tabora Boys na Tabora Girls.

(ii) Wanafunzi 122,908 wakiwemo wasichana 62,731 na wavulana 60,177 wamepangiwa ktk shule 519 za Sekondari za Bweni za Kitaifa za  Kidato cha Tano

(iii) Wanafunzi 5,044 wakiwemo wasichana 2,515 na wavulana 2,529 wamepangwa ktk Shule 11 za Sekondari za Kutwa za Kidato cha Tano.