Raisi Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wa wakala wa usajili, ufilisi na udhamini ambapo;
Amemteua Bw. Frank Kanyusi Frank kuwa kabidhi Wasii mkuu. Kabla ya uteuzi huo Bw. Frank alikuwa Mwanasheria Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Nafasi hiyo ilikuwa ikichukuliwa na Bi. Angela Kemanzi Anatory ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Raisi amemteua pia Bi. Irene Joseph Lesullie kuwa naibu Kabidhi Wasii Mkuu. Kabla ya uteuzi Bi. Lesullie alikuwa Mkurugenzi msaidizi sehemu ya Mashauri ya Kimataifa, ofisi ya wakili mkuu wa serikali
Nafasi hiyo ilikuwa ikichukuliwa na Bi. Lina Robert Sanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa
FOLLOW US HERE