Wafuasi 65 wa dhehebu la mchungaji Mackenzie washtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua

 


Habari zilizoripotiwa kutoka nchini kenya ni kuwa;

Wafuasi 65 wa dhehebu la kidini nchini humo, waliookolewa kutoka msitu wa Shakahola, wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka wakishtakiwa kwa kujaribu kujiua.

Jambo hili ni kinyume na sheria, ikiwa ni pamoja na kumsaidia mtu kujiua, kushindwa kuchukua hatua au kutoripoti kosa pia ni hatia ambayo hukumu yake ni kifungo cha maisha gerezani. 

Mnamo Aprili, polisi walianza kutoa miili kutoka kwa makaburi ya pamoja kutoka katika msitu huo.

Imeripotiwa kuwa mpaka sasa, watu 318 wanaohusishwa na dhehebu hilo wamethibitishwa kufariki na wengine 613 bado hawajulikani walipo

Aliyejiita mchungaji wa kanisa la Good News International Church Paul Mackenzie anadaiwa kuwashawishi watu kufunga hadi kufa, jambo ambalo amelikanusha.

Jambo la ajabu ni kuwa, Washiriki 16 wa dhehebu hilo ambao wako chini ya ulinzi wa polisi wamekuwa wakisusia kula tangu tarehe 4 Juni.

Jambo hilo limepelekea Waendesha mashtaka wa serikali kuamua kuwatenganisha na watuhumiwa wengine, na kulazimishwa kula.