SIMULIZI: Penzi la Clara na Christian (Sehemu ya pili)


 Inaendelea…..

Clara alipofika Ufaransa kwa ajili ya masomo ya masters, aliyafurahia sana mazingira ya kule kwa sababu ya uzuri wa mji ule aliokuwepo (Paris). Mpenzi wake Clara (Christian) alibaki akiwa na huzuni sana huku Tanzania, akiwaza pengine ulaya lolote linaweza kutokea 

Lakini alimuamini sana Clara hivyo akaamini kabisa hatoweza kumsaliti na akirudi watatimiza azimio lao la muda mrefu ambalo ni ndoa.

Clara akiwa katika hali ya ugeni huko Paris alienda moja kwa moja kureport katika chuo ambacho alikuwa amepata. Na alianza masomo mara moja.

katika  chuo hicho walikuwepo vijana wengi wakike na wa kiume, na wazungu na wenye asili ya kiafrika.

Uwepo wa vijana wenye asili ya kiafrika ulimpa faraja sana Clara maana aliona hatoweza kujinyanyapaa maana wenye asili kama yake wapo wengi pale chuoni.

Alikuwa mpweke kiasi, kwa sababu alikuwa hajazoeana na watu bado.

Darasani kwake alikuwepo kijana mmoja mtanashati sana, alikuwa anaitwa Regnards.

Regnards alimuona Clara jinsi anavyojitenga muda mwingi. Alijua kabisa huyo Clara hatakuwa mwenyeji wa Paris kwa muonekano ule

Siku moja aliamua kumfuata mahali anapokaa Clara, na akaamua kukaa pembeni yake. Akamuongelesha kifaransa, lakini Clara akamjibu kwa kiingereza kuwa sikuelewi.

Ndipo Regnards akajua kabisa kuwa mashaka aliyokuwa nayo ilikuwa sahihi na ni kweli kuwa yule mtu ni mgeni pale mjini

Basi alijitambulisha kwake na kumueleza jina lake. Akamwambia Clara kuwa yeye mbali na kuwa mwanafunzi wa hicho chuo lakini pia ni mwenyeji wa hapo Paris. Alizaliwa pale japo wazazi wake ni watu wenye asili ya Cameroon.

Clara alifurahi angalau amepata ‘company’ yake ya kwanza kabisa. Ambapo alifurahi zaidi kuwa company yake ni mtu mwenye asili ya nyumbani. Na jambo hilo ndivyo lilivyokuwa, mara nyingi watu waliokuwa wa company moja walikuwa ni watu wenye asili moja japo haikuwa mara zote.

Regnards alikuwa ni mchangamfu sana. Alielewa kuwa Clara ana upweke kwa sababu ya ugeni aliokuwa nao. Basi akaamua kumfanya ajiskie yukonyumbani. Alimtoa ‘out’ siku hiyo wakapata nafasi ya kunywa kahawa jioni, na kwa vile yale yalikuwa ni majira ya baridi, hiyo kahawa ilinoga sana

Alimtembeza Clara sehemu nyingi za mji huo. Kwa kipindi cha wiki moja mpaka mbili alihakikisha anampeleka sehemu zote maarufu za mji huo. Gharama zote za kila kitu zilikuwa juu yake Regnards, hakika alikuwa kijana mzuri sana.

Clara akazidi sana kuifurahia company yake. Hakuwa msaada mzuri tu kwa maisha nje ya darasa lakini pia hata darasani, alimuomba Clara wawe wanasoma wote, basi wakawa wanasoma wote.

Walikuwa wanafanya kwa zamu, leo wanakutana kwa Reganards kesho kwa Clara au chuoni penyewe.

Uwezo wake darasani Regnards ulikuwa mzuri sana. Hivyo kweli akawa msaada sawasawa kwa Clara.

Ikafika hatua sasa Clara na yeye akawa ameshakuwa mwenyeji wa mji na chuo. Na yeye akawa anamtoa Reganards ‘dates’ za kutosha. Upendo ukabalance sasa (tucheke kidogo)

Sasa siku moja walikuwa na mtihani asubuhi ya saa mbili. Clara alichelewa kulala siku hiyo. Ikafika mpka saa mbili hajafika kwenye chumba cha mtihani. Kabla ya pale Regnards alikuwa ashampigia simu mara nyingi baada ya kuona muda unaenda halafu hatokei, lakini alikuwa hapokei simu. Alimpigia sanaa lakini hapokei. Akajua fika huyu kalala “sasa sijui namsaidiaje”

Clara alikuja kuamka saa tatu na dk hivii akaona ashapoteza hiyo ‘test’.  Hapo ni kujipanga kuongea na ‘professor’ vinginevyo hizo ni story nyingine za kutokuendelea na chuo. Aliwaza sanaa siku hiyo

Baadaye kama saa nne hivii akampigia simu, Regnards akawa analia lia alivyokosa test kijinga. Regnards akamwambia “ mummy nimefanya mtihani mara mbili na nimekusanya. Yaani mmoja wa kwangu na mwingine wa kwako. Nimeweka namba zangu kwenye mtihani wangu na zako kwenye ule Mwingine. Na nimetumia akili katika ukusanyaji. Nikakusanya yote miwili bila professor kugundua. Na hata kusaini kwa ajili ya mahudhurio ya mtihani nimekusignia. Na professor hajajua chochote. Kuwa makini wakati mwingine sasaaa”

Clara hakuamini anachokisikia. Ilikuwa ni ajabu mtu kufanya ‘risk’ kubwa namna ile kwa ajili ya mtu mwingine, labda angekuwa amefanya kwa ajili yake mwenyewe, hapo ingekuwa ni sawa kabisaa.

Ilimpa wakati mgumu sana kumuelewa Regnards ni mtu wa aina gani. Kwa kweli siku hiyo alifurahi sana kukutana na Regnards

Sasa siku moja Regnards alimuuliza Clara kama ana mchumba aliyemuacha huko Africa. Clara akamwambia “ndio ninaye na kiukweli ninampenda sana”, lakini Regnards kwa upande wake yeye alisema hakuwa na mchumba.

Alikuwa naye kabla “lakini saivi kila mtu ana maisha yake” alisema Regnards 

Siku moja Regnards alimueleza Clara juu ya kuwa na hisia na yeye, akamwambia japo alimwambia ana mchumba Africa. Akamwambia bado anahitaji kuwa na mchumba huko Paris walipokuwa. 

Akamwambia “utakuwa huku kwa miaka miwili, ni mingi sana, unahitaji mtu ambaye atakuwa furah yako Kipindi chote utakachokuwa huku na huyo mtu naomba niwe mimi.”

Clara alikataa, akasema hawezi kumsaliti Christian wake. Reganards akamwambia “huyo ni mpenzi wako wa kwenye simu (online boyfriend) kwa sasa. Maana huwezi kumuona mpaka mtafutane whatsap. Unahitaji wa kuwa naye huku, utakayemuona akakupa furaha.”

Clara alikataa kabisa. Akasema “hata unieleze sababu ipi, mimi siko tayari kuwa na mwanaume mwingine zaidi ya huyo unayemuita ‘online boyfriend’”

Regnards aliondoka kwa hasira sana, baada ya kuona amejieleza sanaa halafu mtoto haelewi ‘kachomoa’.  Akamkasirikia kabisa Clara maana yeye binafsi hakuona sababu ya Clara kumkatalia.

Baada ya siku tatu. Regnards yuko nyumbani kwao. Mama yake anamuita atoke chumbani rafiki yake amekuja. Akamwambia “mama huyo Clara mwambie arudi tu.”

Mara mlango wa chumba chake unagonga, akaamua, afungue, Clara huyo akamrukia na kumkumbatia. Kilichofuata ni story za wakubwa

Nini kilisababisha Clara kuamua kumsaliti mpenzi wake Christian, aliyeko Africa? Je, nini hatima ya penzi hili jipya? Christian anajua lolote? Na akijua itakuwaje? Kwanini Clara alishindwa kuvumilia huko Ulaya na wakati aliweza kuvumilia kule chuo kwingine alipokuwa anachukua degree (kama tulivyoona sehwmu ya kwanza)

Tukutane sehemu ya mwisho ya simulizi hii kupata majibu hayo yote.



Imeandikwa na Damas Bayona

Mawasiliano: +255747671795