Feisal “Pesa nitapeleka kwa watoto yatima, msikitini, kanisani na kwa watu wenye uhitaji”

 


Mchezaji Feisal Salum ‘Feitoto’ baada ya kusaini mkataba wake mpya na timu ya Azam FC, amemshukuru Raisi Samia Suluhu kwa jinsi ambavyo aliingilia kati na kuwaomba yanga kumaliza tofauti zao na yeye. Aidha kuhusu pesa ambazo alichangiwa kwa ajili ya kwenda mahakama ya usuluhishi wa michezo (CAS) amesema kiasi hicho kilikuwa ni pesa za kitanzania milioni 9 

Feisal amesema kuhusu pesa hajui ni nani alitoa na nani hakutoa hivyo itakuwa vigumu kujua ni nani wa kumrudishia. Hivyo pesa hizo atazipeleka kwa watoto yatima, msikitini na kanisani na watu wenye uhitaji.