Muswada wa marekebisho ya sheria ya usalama wa taifa wapitishwa rasmi na Bunge

 


Muswada huo ambao unawapa kinga ya hawa usalama wa taifa kutokushtakiwa katika makosa ya jinai pale ambapo makosa yamefanyika katika kutekeleza majukumu yao, bunge limeupitisha tayari kwa ajili ya kutiwa saini na kuwa sheria.

Muswada huu ulizua mjadala ambapo wengi waliona ni kama utaleta uvunjifu wa amani kwa sababu ya kuwapa hawa usalama wa taifa nguvu ya kuua/kuumiza na kutokushtakiwa.

Waziri OR Utumishi mh. Simba Chawene amesema “kinga ni wakati wa kutekeleza majukumu yaliyosemwa kwa mujibu wa sheria ya nchi” amesema Simba Chawene. Aidha amesema kuwa kama Nesi hosipitalini akimchoma mgonjwa sindano halafu mgonjwa akafa anakingiwa basi ni sawa pia na kwa huyu ambaye risasi imefyatuka ikamuumiza mtu wakati wa kupambana na jambazi. 

Lakini pia ameeleza wazi kuwa huyo usalama wa taifa akienda mtaani na akagombana na mtu akaitumia silaha yake vibaya basi sheria haitamkinga mtu wa namna hiyo.