Katika ukurasa wake wa twitter baraza wameandika;
Baraza la uuguzi na ukunga ni mamlaka ya kisheria iliyoanzishwa kwa ajili ya usimamizi wa taaluma na wanataaluma ya uuguzi na ukunga nchini.
Lengo la kianzishwa chombo hiki ni kuhakikisha jamii inapata huduma zilizo bora na salama kutoka kwa wauguzi na wakunga.
Baraza linafanya kazi chini ya Sheria ya uuguzi na ukunga ya mwaka 2010
Baraza limepata taarifa ya muuguzi msajiliwa wa Baraza (jina limehifandhiwa) anayetuhumiwa kumbaka mama mjamzito aliyefika katika Hospitali ya wilaya ya Sikonge , Tabora kwa ajili ya kupata matibabu.
Baraza la uuguzi na ukunga linalaani kitendo hicho, ambacho ni cha kinyama, ukatili uliopitiliz na ni kinyume na maadili ya uuguzi na ukunga
Baraza linatoa pole kwa mama aliyepata madhila hayo, lakini pia baraza linawajulisha umma wa watanzania kuwa baada ya taratibu za uchunguzi Na vyombo vya kisheria kuthibitisha muuguzi huyu kutenda kitendo hicho; baraza litachukua hatua za kinidhamu za kitaaluma kwa mujibu wa kifungu cha (25)(2)(c) cha sheria ya uuguzi na ukunga ya mwaka 2010
Baraza linatoa wito kwa wauguzi na wakunga nchini, kutoa huduma kwa kuzingatia, Utu, taratibu, kanuni na sheria, kwa kuwa matendo kama haya yanaiaibisha taaluma ya wauguzi ambao ni kiungo katika upatikanaji wa huduma bora za matibabu
FOLLOW US HERE