Imeripotiwa kuwa Takriban watu 25 wameuawa katika shule moja magharibi mwa Uganda na waasi wanaohusishwa na kundi la Islamic State.
Watu wengine wanane bado wako katika hali mahututi baada ya kushambuliwa kwa shule ya sekondari ya Lhubirira huko Mpondwe.
Polisi wanasema shambulio hilo la Ijumaa lilitekelezwa na Allied Democratic Forces (ADF) - kundi la Uganda lenye makao yake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Wanajeshi wanafuatilia kundi lililokimbia kuelekea mbuga ya Virunga nchini DRC, polisi waliongeza.

FOLLOW US HERE