Penzi la Clara na Christian (sehemu ya tatu)


 Inaendelea…..
Clara alibaki na mawazo sana baada ya Regnards kuondoka kwa hasira kwa sababu ya kukataliwa na Clara. Aliwaza jinsi ambavyo wamekuwa karibu sana na Regnards na mambo mengi mazuri ambayo Regnards alikuwa akiyafanya kwake. Lakini aliona potelea mbali Yeye atabaki muaminifu kwa Christian.

Ilipita siku ya kwanza nzima, hajapokea simu yoyote kutoka kwa Regnards, haikuwa kawaida na alikuwa ameshamzoea kama rafiki yake wa karibu sana. Na sasa, rafiki kawa kimya siku nzima na wakati wamezoeana sana, alijikuta anammiss

Lakini ‘akavunga’. Ikapita siku ya pili, ikapita ya tatu, Regnards yupo kimya na wala hapokei simu zake.

Clara alijikuta anapata wakati mgumu sana, anapoteza ukaribu wake na Regnards kulinda penzi lake na Christian aliyeko mbali huko Africa.

Sasa, kwa sababu ya namna alivyokuwa anapata Wakati mgumu. Aliona “bhana liwalo na liwe wacha nikamkubalie Regnards, siwezi kuendelea kuvumilia kuwa mbali na yeye kwa sababu ya mtu ambaye hata sijui anafanya nini huko, yawezekana na yeye huko yuko bize na wanawake wengine na mimi hapa sijui najidanganya kulinda penzi”

Alienda kwa Regnards na akafanya kama tulivyoona sehemu iliyopita, na huo ukawa ndio mwanzo wa mahusiano yao. Walipendana sana. Na taratibu Christian akaanza kusahaulika.

Sasa, Kibaya zaidi kilikuja kuwa pale ambapo Regnalds aliamua kumpiga Clara marufuku kuendelea kuchat na Christian, akimwambia hawezi kuwa na Mabwana wawili na sasa aachane kabisa na huyo Christian.

Clara taratibu akaanza kupunguza mawasiliano kwa Christian ; hatariiii

Christian akawa anaona ‘texts’ zinajibiwa siku mbili baada ya kutumwa.

Christian alianza kuogopa kuwa alichokifikiria ni kama kinaanza kutokea. Lakini mara hizo chache ambazo Clara alikuwa akimjibu alikuwa anamwambia yuko bize na masomo ndio sababu ya kuchelewa kujibu ‘message’ 

Christian alilazimika kumuamini. Clara akazidi kula maisha na Regnards. Alienda Ulaya akiwa na msimamo mkali lakini sasa imekuwa habari nyingine.

Sasa ilitokea kule Africa, Yule mdogo wake na Clara ambaye alikuwa hapendi shule, na Clara akamuomba Christian amsaidie kuwa anamuangalia na kumsimamia kwenye masomo yake, alikuwa akitembea barabarani na ghafla gari likatokea upande ambao hakutegemea likamgonga vibaya sana

Mwenye gari alikimbia na gari kama hajaona chochote maana aliona hiyo ishakuwa ni kesi tayari, na ukizingatia alimgonga eneo ambalo halikuwa na watu wengi.

Marafiki zake wawili waliita watu wa kutoa msaada na kijana huyo mdogo akakimbizwa hospitali

Habari zikafikishwa nyumbani. Kijana alipelekwa akiwa mahututi. Alikaa wiki moja na siku kama nne huko mahututi na ndipo alipotolewa na kupelekwa wodini kuendelea na matibabu huku akitakiwa kufungwa chuma kwa ajili ya mifupa iliyovunjika.

Sasa ‘kizaazaa’ kikubwa kilikuwa kwenye gharama za matibabu. Familia haikuwa na hela na gharama za matibabu zilikuwa ni kubwa sana. Walijaribu kila namna kuhangaika kwa ajili ya matibabu lakini hawakuweza.

Christian aliwaza mengi. Akaona bora afanye jambo ambalo ni gumu kwake lakini anusuru maisha ya mdogo wake na mke wake mtarajiwa

Unajua alifanya nini?! Aliamua kwenda kongea na mama yake wauze baadhi ya ‘frame’ walizokuwa nazo kama familia.

Na kwa sababu mama alimpenda mkwe wake aliona hawana budi kufanya hivo kunusuru maisha ya mdogo wake na mkwe wao

Walifanya hivyo na matibabu yalifanyika. Familia ya Clara walimshukuru sana Christian kwa moyo wake wa pekee sana. Na habari hizi zikamfikia Clara kama zilivyo.

Alielezwa hayo na mama yake wakati amempigia ‘voice call’ mida ya usiku. Usiku huo ulikuwa mrefu sana kwa Clara maana aliwaza sana mambo anayomfanyia kwa siri ilihali mtu yuko na moyo wa upendo namna ile.

Alilia sanaa usiku huo. Alitamani ampigie Christian

amuombe msamaha lakini akakumbuka christian hajui chochote. Kuanzia wakati huo akaanza kuonyesha mabadiliko kwa Regnards maana kila alipokuwa akipata ‘message’ kutoka kwa Christian moyo ulikuwa unamuuma sana.

Na hapo ndo tunakuja kuona lile tukio la sehemu ya kwanza ambapo yupo anakumbatiana na Reganards na ghafla message kutoka kwa Christian inaingia, anaondoka na kumuacha Regnards huku akilia. Nafsi yake inajutia sana alichokifanya kwa christian.

Usiku huo anakaa kwa muda mrefu akiwaza na mara akaamua kumpgia simu Regnards nakumwambia, ‘let’s end this’ (tuhitimishe hili)

Regnards hakujibu chochote lakini huo ndio ukawa mwisho wa uhusiano wao, Clara baada ya miezi michache akamaliza ‘masters’ yake na kurudi Africa. Akaendelea maisha na christian kama hakikuwahi kutokea kitu.

Naam, walioana kabisa na maisha yaliendelea

Mwisho wa Simulizi


Imeandikwa na 

Damas Bayona