Ndege iliyokuwa imembeba Raisi wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ambaye ni
kiongozi wa juhudi za maraisi sita wa Afrika ambao wameelekea Ukraine kwa ajili ya kusuruhisha mgogoro wake na Urusi ilizuiliwa na kutua katika uwanja wa ndege wa chopin Warsaw nchini Poland.
Mamlaka husika ya usalama wa Raisi huyo wa Afrika kusini imeripoti kuwa kitendo hicho hakikuwa sawa na ni dalili za ubaguzi wa rangi kwani Raisi na msafara wake wa watu 120 katika ndege hiyo wakiwemo waandishi wa habari walicheleweshwa kufika Kyiv kwa muda ambao walipaswa kufika lakini pia ni kuhatarisha usalama wao. Serikali ya Poland haijazungumza lolote katika hilo, Hata hivyo Ramaphosa hakuzuiliwa kwenda ambapo amefika Kyiv ijumaa asubuhi kwa Treni

FOLLOW US HERE