NINI KIMEMTOKEA EDEN HAZARD?


 Kulingana na chapisho la Club ya Real Madrid katika tovuti yao Eden Hazard ameshinda jumla ya makombe 8 akiwa na Club ya Real Madrid ambayo ni; European cup 1, Club World Cup 1, European Super Cup 1, La Liga titles 2, Copa de Rey 1, na Spanish Super Cup 2. 

Misimu yake minne Santiago Bernabeu imekumbwa na matatizo ya mara kwa mara ya majeraha, na amecheza mechi sita pekee za LaLiga msimu huu ambapo, nne kati ya hizo akitokea benchi bila kufunga bao lolote.


 "Real Madrid C.F. na Eden Hazard wamefikia makubaliano ambapo mchezaji huyo ataachiliwa kutoka kwa klabu mnamo Juni 30, 2023," Club ya Real Madrid ilisema

 “Eden Hazard amekuwa sehemu ya klabu yetu kwa misimu minne, ambapo ameshinda mataji manane: Kombe moja la Ulaya, Kombe la Dunia la Klabu moja, Kombe la Super Super la Ulaya, La liga mbili, Copa del Rey moja na Super Cup mbili za Uhispania.


 "Real Madrid inataka kuonyesha mapenzi yake kwa Eden Hazard na inamtakia kila la heri yeye na familia yake katika kipindi hiki kipya."


 Matatizo ya jeraha ya Hazard yalianza katika msimu wake wa kwanza akiwa Madrid, kwa kuvunjika kifundo cha mguu na kuhitaji kufanyiwa upasuaji na kuingizwa chuma jambo ambalo lilisababisha matatizo zaidi kabla ya kuondolewa miaka miwili baadaye.


 Nahodha huyo wa zamani wa Ubelgiji hakuweza kurejesha ubora wake, na aliona nafasi yake anayopendelea zaidi ya winga ya kushoto ikikaliwa na nyota chipukizi Vinicius Junior.


 Alistaafu kucheza soka la kimataifa mwezi Desemba, baada ya Ubelgiji kufuzu hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia la 2022.


 Mwezi mmoja kabla ya hapo, Hazard aliomba radhi kwa mashabiki wa Real Madrid katika mahojiano na gazeti la Marca, akisema kuwa "amesikitika sana kwa kilichotokea" na kutathmini athari zake uwanjani kama "sifuri," akisema atakubali kuhama msimu huu wa joto.

Hata hivyo amekuwa mchezaji aliyekuwa na mafanikio sana katika club aliyotokea (chelsea) kuelekea Madrid. 

Kulingana na chapisho la tovuti ya club ya chelsea; Hazard alicheza mechi 352 na kufunga magori 110. 

Akiwa na Club ya chelsea alishinda makombe mawili ya EPL ( 2015 & 2017), kombe moja la FA (2018), makombe mawili ya EUROPA (2013 & 2019) 

Mafanikio binafsi akiwa na club hiyo (chelsea) ni pamoja na mchezaji bora wa club (2014, 2015, 2017, 2019)

Gori bora la msimu kwa club yake (2015/2016 aliifunga Tottenham, 2016/2017 aliifunga Arsenal, 2018/2019 aliifunga Liverpool)

Mchezaji bora wa mwaka wa PFA (2015) , mchezaji bora wa EPL (2015), mchezaji bora wa mwaka FWA (2015), mchezaji bora mdogo wa mwaka wa PFA (2014), runner-up wa mchezaji bora wa mwaka wa PFA (2017), runner-up wa mchezaji bora wa mwaka wa FWA (2017)

Mchezaji bora wa nchi ya Ubelgiji (2017), mchezaji bora wa ubelgiji anayecheza nje ya nchi (2017)