Nini kifanyike kukabiliana na ubaguzi wa rangi?


 Ubaguzi wa rangi ‘racism’ ni moja kati ya changamoto kubwa sana ambazo wanakutana nazo wachezaji wengi wenye asili ya kiafrika maarufu kama ‘black people’, ‘people of color’ n.k huko katika timu zao za Ulaya, America na Asia.

Aidha kumekuwa na nchi ambazo kesi hizi zimekithiri pamoja na kuwepo kwa ‘movements’ nyingi ambazo zinapinga ubaguzi wa rangi kama vile ‘black lives matter’ 

Watu wengi wamejitokeza kupiga kulele kwa ajili ya jambo hili la ubaguzi wa rangi, hata hivyo bado linaoneonekana nguvu yake kuendelea kuwepo 

Inaripotiwa kuwepo pia na watu wengi ambao wanaonyeshwa vitendo hivi vya ubaguzi wa rangi ambao hawasemi popote wala kulalamika popote. Na watu hao ni wengi kuliko wale ambao tunawasikia wakilalamika. Aidha ni watu wale waliomaarufu tu ndio ambao huwa tunawasikia, kwa sababu ya kuwa na namba kubwa ya wafuasi katika mitandao ya kijamii, lakini namba ya watu wanaokutana na hili la ubaguzi wa rangi ni kubwa zaidi ya wale tunaowaona kwenye mitandao ya kijamii.

Jambo hili linapelekea watu wengi kuwa na imani kuwa ubaguzi wa rangi hauwezi kuisha. Utaendelea kuwepo labda kupunguza kwa kiasi fulani. Je, ni jambo ambalo tunapaswa tuliamini hivyo tu?

Tukiamua kuamini hivyo, basi hakutakuwa na sababu ya kuendelea kupigania hizi haki za kuheshimiwa bila kujali rangi yako ya ngozi, maana tutakuwa tukifanya kitu ambacho hakiwezekani.

Nguvu kubwa ya kupambana na huu ubaguzi wa rangi ipo kwa raia wa kawaida lakini nguvu kubwa zaidi ipo katika serikali zote. Hapa ninamaanisha serikali ya nchi husika na serikali za mashirika, kampuni na asasi mbalimbali.

Serikali hizi ndizo ambazo zinaweza kuweka sheria za kuwaadhibu watu wote watakao jihusisha na vitendo vya ubaguzi wa rangi

Mwezi uliopita La Liga (Ligi kuu ya mpira Hispania) kulitokea vuguvugu kubwa la ubaguzi wa rangi ambao ulionyeshwa kwa mchezaji wa Real Madrid, Vincius Jr. watu wengi maarufu walipiga sana kelele hatua zichukuliwe kwani imekuwa kawaida sana kwa wachezaji weusi kuonyeshwa vitendo vya ubaguzi wa rangi kwenye ligi hiyo. 

La liga iliripoti kwa serikali ya Hispania watu 7 waliojihusisha na vitendo hivyo na ikaomba nguvu ya sheria ifanye maamuzi juu yao. Hiyo ilikuwa ni kwa sababu kwa sheria za Hispania, La Liga haiwezi kuiwekea vikwazo timu yoyote kwa sababu ya vitendo vya ubaguzi wa rangi aidha La Liga itatakiwa ku ‘identity and report’ kesi za ubaguzi na kilichobaki kitatekelezwa na serikali 

Je, ni sawa kuinyima nguvu taasisi kama hiyo kupinga vitendo hivi vya ubaguzi wa rangi ya kuiwekea moja kwa moja vikwazo timu ile itakayojihusisha na ubaguzi wa rangi? 

Hilo pia limepigiwa kelele na wengi ambao waliweza kufuatilia na kujua. Ipo haja ya kila nchi hasa zile ambazo vitendo hivi vimeshamiri, kuzipa nguvu taasisi kama hizi ambazo vitendo hivi vinafanyika chini yake, ya kuhukumu wahusika sawasawa na sheria zitakazowekwa na taasisi husika. 

Binadamu wote ni sawa. Tofauti za rangi, imani na asili hazitufanyi wote kutokuwa binadamu. Tuna wajibu wa kila mmoja kutetea haki ya usawa kwa watu wote bila kujali tofuti hizo nilizotaja hapo juu.