Marekani na China zaahidiana kuboresha uhusiano wao baada ya mazungumzo


Marekani na China zimeahidiana kuhimarisha uhusiano wao uliokuwa na mivutano baada ya ziara ya siku mbili ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken mjini Beijing.

 Bw Blinken alikutana na Rais Xi Jinping wa China kwa mazungumzo siku ya Jumatatu, akianzisha upya mawasiliano ya kiwango cha juu kati ya mataifa hayo yenye nguvu na yanayovutana.

 Bw Xi alisema wamepiga hatua, huku Bw Blinken akidokeza kuwa pande zote mbili ziko tayari kwa mazungumzo zaidi.

 Lakini mwanadiplomasia mkuu wa Marekani aliweka wazi kuwa bado kuna tofauti kubwa.

 "Nilisisitiza kwamba... mawasiliano endelevu katika ngazi za juu ndiyo njia bora ya kudhibiti tofauti kwa uwajibikaji na kuhakikisha kwamba ushindani wetu hautuingizi kwenye migogoro," Bw Blinken aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano huo wa dakika 35 katika Ukumbi Mkuu wa Watu wa Tiananmen Square 

"Nilisikia vivyo hivyo kutoka kwa wenzangu wa China," alisema.  "Sote wawili tunakubali hitaji la kuhimarisha uhusiano wetu."

 Lakini Bw Blinken, 61, alisema alikuwa na "jicho la umakini" kuhusu Uchina na kulikuwa na "maswala mengi ambayo hatukubaliani nayo kabisa hata kwa nguvu hatukubaliani".

 Uhusiano kati ya Beijing na Washington umedorora kutokana na vita vya kibiashara vya enzi ya Trump, madai ya Beijing dhidi ya Taiwan na kutunguliwa kwa puto (baloon) linalodaiwa kuwa la kijasusi la China juu ya Marekani mapema mwaka huu.

Lakini Bw Xi alipendekeza kuwa uhusiano unaweza kusonga katika mwelekeo mzuri.

 "Pande hizo mbili pia zimepiga hatua na kufikia makubaliano juu ya baadhi ya masuala maalum," alisema, katika nakala ya hotuba yake iliyotolewa na idara ya serikali ya Marekani.  "Hii ni nzuri sana."

 Mkutano na Bw Xi haukuwa kwenye ratiba ya Bw Blinken na ulitangazwa saa moja tu kabla haujafanyika.

 Ingetazamwa na watu wengi kama upuuzi kama haingefanyika, hata hivyo, hasa tangu mwanzilishi mwenza wa Microsoft Bill Gates kukutana na Bw Xi huko Beijing mapema wiki hii.

 Badala yake, Wamarekani wataweza kuashiria ziara ya katibu huyo kama ushirikiano wenye mafanikio na serikali ya China baada ya miezi kadhaa ya mahusiano dhaifu sana.

 Bw Xi pia alikuwa akituma ujumbe kwa watu wake kwamba serikali yake ilikuwa inafikia Washington.

 "Ni muhimu kabisa kuwa na aina hizi za mawasiliano," Bw Blinken alisema.  "Hili ni jambo ambalo tutaendelea kulifanyia kazi."

 Rais wa Marekani Joe Biden na maafisa wa Washington wamesema wanawaona Wachina kama wapinzani na washindani na sio wapinzani.  Ushindani huo unakuwa mzuri maana unaleta ukuaji wa kijeshi na kiuchumi

Chanzo: BBC.com