Jeshi la Polisi lakamata na kuwatawanya waandamanaji leo Juni 19

 


Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya waandamanaji na kuwatawanya wengine katika maandamano maalumu yaliyoitishwa na kijana mwanaharakati Deusdedith Soka.

Maandamano hayo aliyaitisha terehe 15 kupinga mkataba wa uendeshaji na uboreshaji wa bandari uliopo kati ya Dubai na serikali ya Tanzania 

Jeshi la polisi lilitoa tamko la kuzuia maandamano hayo na kutaka utaratibu mwingine wa kuwasilisha maoni na mawazo yao utumike bila kuingilia uhuru wa watu kufanya shughuli zao bila kusumbuliwa.

Hata hivyo wanaharakati hao wakiongozwa na Ndugu Soka hawakuona mantiki ya zuio hilo kwani ni kinyume na haki yao ya kikatiba maana yaliitishwa maandamano ya amani na sio vurugu. Nia yao ya kuendelea na maandamano ikabaki palepale

Wanaharakati hao wanapinga mkataba huo kwa kile ambacho wanakizungumza wengi wao kuwa mapungufu ya huo mkataba.

Katika Post zao nyingi katika mitandao ya kijamii walionyesha sababu za maandamano hayo ambazo zilikuwa ni kupinga mkataba huo ambao waliuzungumza kuwa uliwapa hao DP World ya dubai umiliki wa milele wa bandari hiyo kwani mkataba haukuonyesha ukomo wa mkataba huo lakini pia kuna vifungu katika mkataba huo ambavyo vinaizuia Tanzania kwa sababu yoyote ile kujitoa katika mkataba huo na mengine mengi