Ameandika msemaji wa Simba SC Ahmed Ally;
Muda umetenganisha mapenzi yetu na Jonas Mkude. Ameondoka mtu tunaempenda kweli, ameondoka Mtoto wetu, mtoto wa nyumbani kwetu . Kwa miaka ya hivi karibuni hakuna mchezaji tumewahi kumpenda kama Jonas Mkude na tutaendelea kumpenda
Wakati Simba ina njaa, Azam ilimhitaji hakuenda, UTO walimtaka hakuenda. akachagua kuvumilia njaa yetu huyu ni zaidi ya mchezaji kwetu
Sisi tulitamani Jonas Mkude amalizie mpira wake Simba kwani hatutaki kucheza nae akiwa timu nyingine, Kwa sababu tukimfunga ataumia na yeye akitufunga ataumia hatuko tayari kumuumiza Mkude wetu
Tumetoa taarifa ya kuachana nae punde tutatoa taarifa ya kumuaga na tutamuaga kwa heshima zote. Sisi ndo tunatambua zaidi heshima ya Mkude kuliko mtu mwingine yeyote na tutamuaga kwa heshima hiyo hiyo
Kila la heri Legend @jonasmkude20

FOLLOW US HERE