Mwanamke aliyempiga Risasi Dereva wake wa Uber amesema kuwa alidhani anatekwa

 



Mwanamke mmoja huko Marekani alimpiga risasi na kumuua dereva wake wa Uber huko El Paso, Texas, baada ya kudhani kimakosa kuwa alikuwa anatekwa na kupelekwa Mexico. 

Dereva, Daniel Piedra, mwenye miaka 52, alipigwa risasi mara kadhaa nyuma ya kichwa mnamo Juni 16 na akafa wiki moja baadaye wakati familia yake ilipoamua kusimamisha msaada wa maisha (machine maalum kwa ajili ya kumsaidia mtu kupumua) 

Alikuwa dereva wa Uber kwa wiki tatu tu na alipenda kukutana na watu wapya. Mpwa wake, Didi Lopez, alisema alikuwa mtu mcheshi, mwenye huruma na mwenye bidii ambaye hakustahili kufa.

Mwanamke, Phoebe Copas, yuko jela na anashtakiwa kwa mauaji. Aliambia polisi kwamba aliona alama ya Juárez, jiji la Mexico karibu na El Paso, na akaingiwa na hofu kwa sababu alidhani alikuwa anatekwa. 


Hata hivyo, polisi walisema hakukuwa na dalili ya utekaji nyara na kwamba dereva alifuata njia yake ya kumpeleka hadi kasino. 


Hakuita msaada au kujaribu kusimamisha gari kabla ya kumpiga risasi dereva. Pia alichukua picha yake na kumtumia mpenzi wake, kulingana na nyaraka za korti.


Katika Ufyatulianaji risasi mwanamke huyo ni mmoja wa wengi ambao wametokea nchini Marekani mwaka huu, ambapo bunduki ni rahisi kupata na sheria ni dhaifu. 


Watu wengi wameuawa au kujeruhiwa na vurugu za bunduki wakati wanafanya shughuli zao za kawaida. 


Ufyatulianaji risasi pia unaonyesha hatari ambazo madereva wa Uber wanakabiliwa nazo kutoka kwa abiria wao.


Familia ya Piedra imeanza kampeni ya ukusanyaji fedha mtandaoni kulipia gharama zake za matibabu na mazishi. Wamepokea takriban dola 70,000 za Marekani kama michango hadi sasa.