Luka Modric aongeza mkataba Real Madrid




Luka Modric amekubaliana na Real Madrid kwa mkataba mpya wa mwaka mmoja ambao utamweka katika klabu hiyo hadi msimu wa joto wa 2024. 

Modric, kiungo wa kati kutoka Croatia, ambaye alikuwa karibu kumaliza kandarasi yake na Bernabeur, alikuwa akitajwa kuwa anaweza kuhamia Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

 Modric, mwenye umri wa miaka 37, amecheza jumla ya mechi 488 na Real Madrid, akiishinda dLa Liga mara tatu na Ligi ya Mabingwa mara tano tangu ajiunge na klabu hiyo kutoka Tottenham mwaka 2012. 

Pia, alishinda tuzo ya Ballon d'Or mwaka 2018 wakati timu ya taifa ya Croatia ilipofika fainali ya Kombe la Dunia.