Movie yoyote itakayo tengenezwa huko Hollywood ni lazima ipitie hatua hizi kuu tano
1. Development: Hapa kwenye hii hatua wanajikita kwenye Uvumbuzi wa wazo/kisa, ununuzi wa hakimiliki ya idea, Uandishi wa Script na proposal,kufanya reseach na film drafting
2. Pre-production: Maandalizi ya kushoot yanaanza kufanyika, waigizaji wanakodiwa na location zinawekewa booking, inaandaliwa na mikataba
Kwa ulaya, kampuni ya filamu au mhusika mkuu nyuma ya project huwa mara nyingi anachukua mkopo benki, utambue kuwa asilimia kubwa ya bajeti za movie za hollywood huwa zinakuwa ‘funded’ na benki, halafu wanakuja kulipana baadae.
03. Production: shooting, hapa watu wanasoma kwanza story darasani kisha wanaingia ‘location’ kuigiza. Hili ni zoezi linaochukua muda mrefu maana ndio kiini cha movie inayotengenezwa
04. Post-production: Hapa ni uhariri wa vipande vilivyoigizwa, picha, sauti na ‘visual effects’ vyote vinawekwa pamoja. Hollywood ndo wamewekeza hapa kuliko sehemu yoyote kwenye ‘Industry’ ya utengenezaji movie . Eneo hili lina hitaji wataalam wengi hapo katikati: kama ifuatavyo
‘Special Effects Artist’ - Kazi yake ni kutengeneza ‘physical effects’, yaweza kuwa ni kinyago kinachofanana na muigizaji ili kitumike kwenye scenes ambazo actor hawezi kuigiza, mfano kukanyagwa na treni au kujirusha gorofani
Modeller: Huyu ni anaye chora na kuumba kidijitali kiumbe chochote mfano; Ghollum kwenye movie ya 'Lord of the Rings' au yule sokwe King Kong kwenye movie ya ‘King Kong’
Animator: Huyu kazi yake ni kumpa uhai Model mfano; Ghollum kwenye 'Lord of the Rings' au yule sokwe King Kong kwenye movie ya King Kong, yaani atembee, aongee, na kuigiza kama vile mtu (muigizaji) wa kawaida ambavyo angefanya.
Compositor: Kazi yake ni kumnyofoa muigizaji aliyeigiza vitendo vya Model kwenye ‘live action scene (footage/clip)’ na kumpachika Model. Pia kazi yake ni kufanya ‘integration’ yaani digital actor aonekane ni real ndani ya clip, aonekane ni kama vile alifanyiwa shooting
Motion Capture Actor - Kama movie itakuwa ni sci-fi huyu actor kazi yake ni kuigiza vitendo ambavyo digital actor (animated model) ambaye atavaa uhusika wa binadamu kwenye movie
Editor: Kazi yake ni kuzikata kata clips na kuzipangilia ili iwe ni stori, bila hatua hii hizo visual effects na special effects havina maana
Mwisho
Distribution: Movie inatoka, inasambazwa na kuanza kuonyeshwa

FOLLOW US HERE