Mwanafunzi Esther aelezea sababu za kukimbia shuleni

 


Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18, Esther Noah, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Panda Hill, ameelezea sababu ya kukimbia shuleni kuwa ni kwa sababu alinyanyaswa kingono na mwalimu anayejulikana kwa jina la Mwalimu Jimmy.

Akizungumza na Habari Digital, Esther amedai kuwa mwalimu huyo alikuwa anamshawishi kimapenzi, na baada ya kumkataa, alianza kumtendea unyanyasaji kwa kumpiga na kisha kumbaka bwenini, akimzuia kutoa sauti za kuomba msaada kwa kumfunga kwa blanketi.


"Baada ya kurudi kutoka kupata chakula, tulienda bwenini kwa kuchelewa, tukala chakula na kisha nikaenda kuoga. Niliporudi bwenini, walimu wengine walikuwa wametutimua kwa sababu tulikuwa tumekwenda kuchukua chakula baada ya muda uliopangwa. Wakati nilipokuwa napaka mafuta, mwalimu [Jimmy] alikuja ndani na kuanza kunipiga baada ya kumwambia kwamba nilichelewa kuchukua chakula. Kisha akaniabaka," ameeleza Esther.


Ameongeza kuwa siku iliyofuata baada ya tukio la ubakaji, wakati wakiendelea na mitihani, walimtuhumu kuwa ameingiza kitabu kwenye chumba cha mtihani ambacho kilikuwa chini ya dawati lake. Kisha alishambuliwa na walimu na kuchaniwa mtihani, licha ya kujitetea kuwa hakuwa na hatia.


"Ilikuwa lazima niende kliniki ya shule, na baada ya kumaliza mtihani wa pili, nilienda kanisani. Nilikuwa nikilia sana kwa nini nilifanyiwa kitendo kile jana na leo ninafunguliwa mashtaka? Nikaamua kukimbia shuleni. Niliandika barua nikiwa na hisia kali na maumivu na nikaondoka mahali ambapo sijulikani," amesema.


Mbali na hayo, kuhusu kijana muuza mkaa anayejulikana kwa jina la 'Baba Jose', ambaye alimtambulisha kama mke wake kwa mwanamke ambaye Esther alikutwa akiishi nyumbani kwake, mwanafunzi huyo alidai kuwa kijana huyo alimpeleka kwa mwanamke huyo ili kumsaidia kupata kazi, na baada ya hapo hawakukutana tena.


Esther na familia yake wamemwomba Serikali kuchukua hatua dhidi ya mwalimu huyo ili kukomesha vitendo vya unyanyasaji na ubakaji vinavyofanywa na baadhi ya walimu.


Unaweza kutufollow katika mitandao yetu hapa chini 👇


Instagram
Twitter
YouTube
TikTok
Facebook