Waziri Kairuki atoa pongezi

 


Ofisi ya TAMISEMI imeripoti;

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi TAMISEMI Mhe.Angela Kairuki ameishukuru Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson (Henry Jackson Foundation for Medical Research International) kwa kuunga mkono jitihada za Serikali.

Mhe. Kairuki amesema, Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Tanzania inadhibiti janga la UKIMWI kupitia kinga, matunzo, matibabu ya VVU na utoaji wa msaada kwa watu wanaoishi na VVU.

Mhe. Kairuki ametoa pongezi hizo kwa Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kimataifa wa Matibabu ya Henry Jackson, Meja Generali Mstaafu Dkt. Joseph Caravalho aliyemtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma leo.