Ronaldo aweka rekodi: mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi na timu ya taifa

 


Siku ya jana Juni 20,

 CRISTIANO Ronaldo ameweka rekodi nyingine kwenye soka baada ya kuwa mchezaji wa kiume wa kwanza kucheza mechi nyingi zaidi katika timu ya taifa.

Ronaldo jana ameichezea Ureno mchezo wake wa 200 wakati wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya mataifa ya Ulaya kwa mwaka 2024  (UEFA EURO-2024) dhidi ya Iceland na kuweka rekodi mpya kwenye soka  la Ureno na ulimwenguni kwa ujumla.

Rekodi hiyo imemfanya nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno kuingia kwenye kitabu cha rekodi za kipekee ( Guinness World Records book)

Ronaldo ameichezea timu ya taifa ya Ureno kwa zaidi ya miaka 20 tangu alipoanza kuichezea Agosti 2003.