Raisi Samia Suluhu Hassan akizungumza katika mkutano wa 14 wa baraza la biashara (TNBC) Ikulu Dar es salaam amesema kuwa kazi kubwa imeendelea kufanyika katika kuboresha mifumo ya TEHAMA kwenye Sekta za UMMA ambapo mifumo wakati wote imekuwa haisomani wala taarifa hazioani. Aidha amesema kuwa kazi kubwa zaidi inaenda kufanyika ambapo mifumo inaenda kusomana na kuwa na vigezo vya kimataifa. Ameongeza pia kuwa changamoto zilizotolewa za Kariakoo ni kwa sababu ya mifumo haijaweza kuchukua taarifa zote hizo na kazi iliyopo sasa ni kuhakikisha mifumo yetu inaweza kubeba taarifa zote zile ili kuweza kuwa na taarifa nyingi ambazo zitaweza kuchukuliwa maamuzi
Akaongezea zaidi na kusema kuwa anawaahidi wananchi kuwa si zaidi ya miezi sita kitakachokuwa kinatokea bandarini atakuwa anaweza kukisoma akiwa Ikulu kwake

FOLLOW US HERE