Maandamano jumatatu 19/06 yapigwa marufuku na jeshi la Polisi

 


Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limepiga marufuku maandamano yaliyoitishwa na kijana kwa jina la Deusdedith Soka ambaye ni mwanaharakati wa haki za binadamu kuelekea Ikulu yakiwa na lengo la kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na DP World  

Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Jumanne Mulilo ameviambia vyombo vya habari kuwa maandamano hayo yamepigwa marufuku na jeshi la polisi na anawataadharisha wananchi kutoshiriki maandamano hayo kwani mtu huyo (aliyeitisha maandamano) kama atakuwa na maoni/hoja zake basi atapaswa kuwasilisha katika vyombo husika ili haki zingine za wananchi kufanya shughuli zao wakiwa huru zisiingiliwe

Taarifa hiyo imetolewa leo ikiwa ni siku moja kabla ya siku ya maandamano hayo ambayo ni jumatatu tarehe 19/06/2023