Luis Suarez “sijui kuhusu Neymar, lakini mimi na Messi tutakuwa wote pamoja”


  “Tulikubaliana pia kuhusu hilo na Neymar. Tunatumai kutumia siku za mwisho za maisha yetu ya mpira katika Club moja.  Kufurahia zaidi furaha ya mpira wa miguu na kucheza kandanda kama tunavyopenda na kustaafu pamoja. Sijui kuhusu Neymar, lakini Messi na mimi bila shaka tutakuwepo pamoja." Alisema Luis Suarez

Kauli hii imegusa mioyo ya wanasoka wengi wapenzi wa hao wachezaji watatu kwani wanatamani kuwatazama tena pamoja. Na kuona ule urafiki na ushirikiano wa Messi, Suarez, na Neymar ndani na nje ya uwanja kwani ulikuwa moja ya mambo mazuri ambayo mashabiki hao wamewahi kuyaona ndani ya soka.