HIZI APA DALILI NA SABABU ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME


Hakikisha unasoma kwa  umakini somo hili, Kwanza fahamu kuwa hakuna alie zaliwa na tatizo la nguvu za kiume. Bali sababu zilizo nyingi nikujitafutia tu mwenyewe.

Tatizo hili huwanyima  watu wengi raha na kupelekea kuwa na mawazo, migogoro katika mahusiano. 

Watu wenye changamoto hii mara zote wanahitaji dawa zisizo na madhara (virutubisho lishe) vilivyotokana na mimea na matunda na kubadilisha mtindo wa maisha.

● DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME:

1. Kukosa Hamu Ya Kufanya  Tendo La Ndoa.

》Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanaume ni moja wapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume na linaweza kusababishwa na sababu nyingi sana. 

》Sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au kisaikolojia au za mchanganyiko wa sababu za kimaumbile na sababu za kisaikolojia.

● BAADHI YA SABABU ZA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA TENDO.

☆ Msongo Wa Mawazo (Depression).

☆ Matumizi Ya Madawa Na Pombe.

☆ Mahusiano Yaliyopo Baina Ya Mwanaume Na Mwanamke.

☆ Matatizo ya kiafya ya muda mrefu (chronic diseases)

2. Kutokuwa Na Uwezo Wa Kurudia Tendo La Ndoa Zaidi Ya Mara Moja.

》Mwanaume mwenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume  akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakua hana uwezo tena wa kurudia mshindo mwingine. Hali hii husababishwa na kutokuwepo na mshukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume. (Nimesha wai elezea juu ya hili)

3.Kutokuwa  Na Uwezo Wa Kusimamisha Uume Kabisa.

》Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume ambayo ndio huufanya uume usimame barabara.

》Kwa kawaida uume wa mwanaume asie na tatizo unaposimama, hutakiwa kuwa imara kama wakati wote wa tendo, lakini kwa mwanaume mwenye changamoto ya upungufu za nguvu za kiume uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na unaweza kusinyaa wakati wowote.

4. Kuwahi Kufika Kileleni.

》Kuwahi kufika kileleni ni hali ambayo inampata mwanaume mwenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume ambapo hutoa shahawa kabla ya kuanza tendo la ndoa au muda mfupi tu baada ya kuanza tendo la ndoa, bila yeye mwenyewe kukusudia.

》Kwa kawaida mtu mwenye tatizo la kuwahi kufika kileleni hutoa mbegu zake za kiume hata baada ya maandalizi kidogo sana.

5. Kuchoka Sana Baada Ya Tendo La Ndoa.

》Hii ni moja wapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume. Hali hii huwapata wanaume wenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume ambayo wakati mwingine huambatana na usingizi mzito mara baada yakumaliza tendo

6. Kuhisi Maumivu Wakati Wa Tendo La Ndoa au mara baada Ya Tendo La Ndoa.

》Hii pia ni moja wapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume, hali hii huweza kuchangiwa na kauthirika kwa tishu za uume ambazo hutokana na upigaji wa punyeto kupita kiasi.

Twende pamoja 🤝 💊⚖

7. Kuchelewa  Sana Kufika Kileleni au Kushindwa Kufika Kileleni Kabisa.

》Ni ile hali ya mwanaume kuchukua muda mrefu kutoa manii wakati wa kushiriki tendo la ndoa, Halihiyo ni tatizo kubwa sana udhani uko vizuri na kujipa moyo.

》Kwa kawaida mwanaume anatakiwa afike kileleni/kutoa manii kwa muda usiozidi dakika 30 wakati wa kushiriki tendo la ndoa. 

》Kwa hiyo mwanaume anaposhiriki tendo la ndoa na kuchukua muda mrefu bila kufika kileleni anahitaji uchunguzi ili kubaini chanzo cha tatizo.

● SABABU ZA UPUNGUFU WA  NGUVU ZA KIUME:

Zifuatazo ni baadhi ya sababu za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume;

》Uzito kupita kiasi na unene uliozidi.

》Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi.

》Uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe.

》Kuwa na mawazo na wasi wasi.

》Kuwa na tatizo la kibofu cha mkojo.

》Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibu magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, kisukari, presha, magonjwa ya moyo nk.

》Tabia za kujichua kwa muda mrefu ( Upigaji wa punyeto)

》Umri hasa wazee 45>.

NB: Katika makala hii tumeona  Dalili na sababu za upungufu wa nguvu zakiume, usipange kukosa somo lijalo "JINSI YA KUTATUA TATIZO HILI". 

Imeandikwa na Mr. Health 

Anapatikana hapa 👇 unaweza ku click

Mr. Health on TikTok