Hii hapa barua iliyotolewa na TFF leo Juni 20

 


TAARIFA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawakumbusha wanafamilia ya mpira wa miguu kuwa ni kosa kushirikiana na wadau ambao wamefungiwa.

Ni muhimu kuzingatia kuwa wadau husika wamefungiwa baada ya kwenda kinyume na Katiba, Kanuni na taratibu zinazosimamia mpira wa miguu.

Hivyo, TFF inaendelea kufuatilia ukiukaji huo ili kuchukua hatua stahiki.

Wanafamilia wote wanao wajibu wa kuheshimu Katiba, kanuni na taratibu zinazotawala mpira wa miguu.

Pia waliofungiwa wanajiweka katika hatari ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu iwapo hawatatumikia adhabu zao kikamilifu.

Cliford Mario Ndimbo

Ofisa Habari na Mawasiliano, TFF

Juni 20, 2023