Alichokiandika Nabi kuhusu kuondoka kwake Yanga


 Amendika hivii;

Habari za jioni 

ningependa kufafanua mambo machache.  uamuzi wangu kuhusu mustakabali wangu na yanga sc ulichukuliwa na kutangazwa kwa klabu mara tu baada ya mechi dhidi ya TP Mazembe.  wakati huo sikuwa na ofa kutoka kwa klabu nyingine yoyote.  

Taarifa kutoka kwenye kituo fulani cha redio kwamba mwanangu alikuwa wakala wangu na amekuja kukamilisha deal ni uongo na upuuzi mtupu.  mwanangu ni mwanafunzi na supporter wa klabu, na alikuja kusupport timu na baba yake, uwepo wake ulikuwa hapo tu kwa sababu hizi, timu yake na baba yake.  

Ningependa pia kusema sikuwahi kukaa na klabu kujadili uwezekano wa kuongeza mkataba, kwa sababu klabu ilijua maamuzi yangu mwezi mmoja uliopita.  Nimehuzunika kama mashabiki wetu wote wapendwa kufikia mwisho wa ushirikiano wangu na klabu.  Nje na heshima kwangu, ningeomba familia yangu iachwe, hasa mwanangu ambaye hana uhusiano wowote na maamuzi yangu ya kikazi 

Asante 

Nesreddine Nabi.