SIMULIZI: WAKALA WA SHETANI




Mgaga wa kienyeji aliishi kanisani, alitumika kanisani.

Akajificha humo.

Sijui ni kitu gani alikuwa anakifikiria.

Sijui kwanini aliamua kutokukaa kwenye makazi yake kama mganga.

Na kwanini akimbilie kutumika kanisani?!


Alikuja kama muumini wa kawaida.

Aliingia ibada imeshaanza akafika na kukaa kwenye kiti pamoja na waumini wengine.

Baada ya ibada kuisha, walikaribishwa wageni na yeye akasimama kujitambulisha.

Akasema yeye amekuja hapo mjini akitokea mji mwingine

Na amekuja huko kwa ajili ya biashara zake. Na ana mipango ya kuendelea kukaa huko. Hivyo ataomba kuwa muumini wa kanisa hilo

Watu wote walifurahi kwa sababu wamepata mgeni mpya ndani ya kanisa. Ni jambo jema.

Alisajiliwa ndani ya database ya kanisa na kuwa mmoja wa waumini wa kanisa hilo.

Alikuwa na moyo mkubwa sana wa utumishi na alijitoa kwa ajili ya mambo mengi sanaa ndani ya kanisa


Kutokana na uwezo wake pia wa kifedha aliokuwa nao, alipata majukumu mengi zaidi aliyokuwa akipewa.

Kwa sababu walijua ukitokea upungufu fulani atamalizia

Ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa kanisa na akapata nafasi ya kuwa kiongozi fulani wa nafasi kubwa katika

kanisa hilo.



Watu walimpongeza na walijivunia yeye kuwa kiongozi wao kwa sababu ya moyo wa kutumika aliokuwa nao.

Kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kifedha pia alikuwa anawasaidia watu sanaaa ndani ya kanisa lile

katika matatizo yao binafsi ya kifedha. Kama kulipa ada za watoto wao, mitaji ya biashara na matatizo mengine yaliyokuwa yakijitokeza.


Na kwa sababu hiyo alijikuta anakuwa mtu wa karibu zaidi kwa mchungaji wa kanisa lile. Kwani hata nyumba ya mchungaji aliirekebisha na kuikarabati

vizuri akanunua gari pia kwa ajili ya mchungaji

Na alijitolea kwa mambo mengi ya kuisaidia familia ya mchungaji

Hakuna jumapili aliyokosa kanisani. Kama ilitokea basi ilikuwa ni mara chache sanaaa. 

Na kwa sababu maalum ambayo aliitoa kabla na watu wakajua.

Alikuwa amenunua nyumba moja ya kifahari katika mji

huo, ila hakuwa na mke wala watoto.

Jambo hilo liliwafanya watu waliohitaji msaada wake kwenda pale muda wowote wanaotaka na kumpata.



Lakini kubwa zaidi lilikuwa likiwashangaza, ni kwa namna gani huyo mtu mwenye maisha mazuri namna hii, anashindwa kuwa na familia.

Mara nyingi alikuwa akiwajibu kuwa familia sio kipaumbele chake.

Yeye kipaumbele chake ni kumtumikia Mungu kwa uaminifu.

Alikuwa akijitetea kuwa yeye ameamua kuishi kama mtume Paulo kwenye biblia ili mke na familia visiwe vizuizi vya yeye kumtumikia Mungu.



Na kwa sababu swala la kuwa na familia ni hiari hivyo alisema kuwa aliamua kuachana nalo Jambo hilo hata mchungaji hakufurahishwa nalo.

Alikuwa akiongea naye mara kwa mara, huku akimuuliza kuwa utajiri wake sasa na biashara zake atavirithisha kwa nani kama hataki familia

Na yeye alimjibu watavirithi watu sahihi hana wasiwasi na hilo.



Sasa, Mchungaji alikuwa na binti yake aliyekuwa na miaka 26 na wakati huo huyo jamaa alikuwa na miaka 40+

Hivyo mchungaji akawa anaona hiyo ni kama fursa ya mtoto wake kumpata mwanaume mzuri maana zaidi ya yote ni mtumishi mzuri sana kanisani



Alijaribu kuongea naye tena, akimwambia kuwa, kwa tabia na mwenendo na imani yake aliyonayo, anafaa sana kuwa mume wa binti yake.

Lakini hilo jamaa yeye hakutaka kuliskia kabisa.

Basi mchungaji akaona isiwe tabu akaamua kumuacha



Lakini jambo hilo lilimuhuzunisha sana binti wa mchungaji kwa sababu alijiona yeye ni mzuri na ana kila sifa njema na wanaume wengi walimpenda. Sasa

akajiuliza huyu mtu anashida gani?!

Akawaza kutokukata tamaa akiamini kuwa mwanamke akikutaka atakupata tu.



Na kwa sababu maisha ya mjini huwa sio kufuatiliana sana, hakuna aliyejua vizuri asili ya huyo jamaa.

Alichowaambiatu ni kuwa yeye ni mwenyeji wa eneo fulani ambalo alilitaja. Na amekuja huko kwa ajili ya

biashara na atakaa na kuweka makazi huko.

Kuna baadhi wachache walitaka kujua na kufika alikotoka ili wakawaone ndugu zake, lakini hakuwapa ushirikiano wakaachana nalo. Japo hawakuhisi jambo lolote la tofauti zaidi ya kuona tu kuwa ni maringo kwa sababu ni tajiri.


Huyo binti wa mchungaji aliitwa Joselina.

Na huyo jamaa jina alilojitambulisha kwao ni Nickson

Joselina alienda akawaeleza marafiki zake jinsi ambavyo huyo Nickson amemkataa. Marafiki zake

wao walikuwa wanatazama pesa tu, hivyo walimwambia asikubali kuachia hizo pesa ziende

Na hapo ndipo rafiki yake mmoja alimuita na kumnong’oneza ushauri fulani hivii ambao hata yeye alishtuka aliposkia. Ila wakamuambia aache ujinga fursa hazijawahi kuja mara mbili akipoteza moja ndo hatokuja kupata nyingine tena. Akaambiwa hapo aweke mambo ya utoto wa mchungaji pembeni kwanza na azingatie ushauri aliopewa.


Ni ushauri gani huu amepewa? 

Je, atafanikiwa kweli au lah?

Nini kinafuata?


Ngoja tuone 

Unaweza kupata break fupi kwa ajili ya sehemu ya pili



SEHEMU YA PILI 


Basi Joselina aliamua kuusikiliza na kuufuata ushauri huo aliopewa na rafiki zake.


Na sasa baada ya Joselina kuamua kufuata ushauri aliopewa na

Rafiki yake ili kuuteka moyo wa Nickson

Akaamua kumkaribisha Nicksoni nyumbani kwao (kwa mchungaji)

Na kwa sababu Nickson aliona ameitwa na mtoto wa mchungaji na pia nyumbani kwake na mchungaji hakusita hata kidogo kwenda.


Alifika pale kwao na mchungaji, na Joselina akamkaribisha na kumpa kahawa.

Nicky hakusita kuchukua kahawa na kunywa. 

Sasa wakati akinywa alianza kusikia usingizi mzito na mara kichwa kizito dakika mbili zilikuwa nyingi, alikuwa

ameshazima tayari.

Kumbe Joselina kwa kufuata ushauri wa rafiki yake, alimpa Nicksoni dawa za kulevya alizopewa na huyo huyo rafiki yake na kuziweka kwenye kahawa.



Kwa hiyo Nickie akalewa na usingizi mzito ukamchukua.

Joselina akamchukua na kumpeleka chumba cha wageni. Halafu akamsearch mfukoni na kuchukua

fungua za gari akaenda kufungua ndani ya gari akachukua funguo za nyumba

Ya Nickson. 

Kwani alijua alipokuwa akiziweka.



Alichukua haraka haraka akaenda kuchongesha kama baada ya muda hivi akarudi na copy yake, wakati huo

Nickson bado yuko hoi humo ndani.

Na familia (baba mchungaji na mama mchungaji hawakuwepo siku hiyo)


Baadaye Nickson aliamka akiwa na fahamu zake akawa anashangaa nini kimetokea mpaka akawa amelala vile.

Rakini Joselina naye akajifanya kumshangaa pia, akamwambia “mimi nilikuona unaanza kusinzia nikakuomba kukupeleka chumbani ukakubali.” 



Sasa kwa sababu huyu ni mtoto wa kike, Nicky hakuona haja ya kuendelea na mabishano kwanza ni aibu alivyolala vile.

Hivyo aliondoka, akafika kwake kama mida ya saa kumi na moja hivi, 

Akaoga na kujiweka sawa.

Akaelekea kwenye mishe mishe zake kama mfanya biashara.



Basi kama mida ya saa mbili hivii usikJoselina alienda kwake, sasa kumbuka ana copy ya ufunguo. 

Hivyo alifungua na kuingia ndani mpaka chumbani kwa Nickson. Akakaa huko, ilivofika kama mida ya saa nne hivi usiku; Alimsikia Nickson akija, akamsikia akifungua mlango na kuingia ndani.

Sasa akawa anamsubiria chumbani

Moyoni akifikiria kabisa kuwa “leo Nickson hachomoki. Na ndoto yangu ya kuolewa na yeye itatimia” 



Sasa, alishangaa mbona muda umekuwa mrefu tangu Nicky

kaingia lakini hamuoni akija chumbani alikomsubiri amfanyie surprise 



Ikabidi ainuke na kwenda kumfuata huko huko sebuleni, hii surprise imeshapanda mtumbwi wa

vibwengo mpaka sasa 😄

Wanasema ukistaajabu ya Musa; Anashangaa anafungua mlango wa chumba haufunguki, anajaribu kuuvuta ni uko locked, anashangaa kwani hakuulock na wala hana funguo za

chumba


Anapigwa na butwaa kubwa

Anaamua kumuita sasa Nickson

Anamuita anashangaa sauti haitoki ndani ya chumba.

Yaani ile unaongea halafu unasikia kabisa hii sauti inaishia hapa hapa haitoki nje.

Hofu kubwa ikamuingia akaanza kupiga kelele lakini anasikia kabisa zinaishia humo humo ndani.


Kibaya zaidi akisikiliza kwa nje ya chumba anamsikia Nickson ni kama anaongea na mtu. 

Halafu wanaongea ‘non-stop’ 

Ikabidi agonge mlango. Wanasema ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni, Mlango ulikuwa hautoi sauti

kabisaaaaa

Alijiskia kama roho inachomoka kwa hofu. Wakati huo taa ya humo chumbani ilikuwa iko on.

Na ghafla ikazima

Hapo ndo alipojiskia kufa, maana alijaribu kusogelea soketi ili awashe tena labda soketi imejizima,

anashangaa soketi haipo. 

Yaani sehemu ya soketi anaona ni flat kama sehemu nyingine



Akiwa kama nusu mfu nusu mtu. Taa iliwaka tena.

Akaangalia soketi ipo, yaani imerudi. Kupiga kelele akashangaa zinatoka akakimbilia mlango ukafunguka,

hakuamini.

Alitoka mbio, cha ajabu sebulen hakuna mtu wala nini.

Anaenda kufungua mlango wa kutoka nje uko locked, kama alivouacha. 

Sasa kimbembe kinakuwa kurudi tena chumbani kuchukua ufunguo atoke. Anaogopa vibaya mnoo.

Hata ungekuwa wewe, ungeweza kweli kurudi tena huko chumbani? 

Alikaa hapo sebuleni anaangalia saa ni

saa nane za usiku imeshafika.

Akaona hawezi kuendelea kubaki humo, bora liwalo na liwe lakini arudi chumbani kuchukua ufunguo.

Alirudi akakuta kupo kama alivopaacha, akachukua ufunguo akatoka kwa speed ya cheetah 🐆 mpaka

sebuleni, akafungua mlango haraka huyoo nje.


Heheheheee! Anashangaa hata nje hilo gari la Nickson alilolisikia limeingia halipo. Kiufupi hakukuwa na gari lolote.

Alienda mbio mpaka kwao ambapo kulikuwa na umbali kama wa km 4 mpaka 5 hivii

Alifika kwao na kugonga mlango kwa nguvu, mama yake akamfungulia, akaingia ndani.

Sasa kwa butwaa aliyokuwa nayo. Ikabidi amuombe mama yake alale naye chumba kimoja maana alikuwa

anaogopa mnoo.

Mama mchungaji akawa anashangaa ni kitu gani kinaendelea kwa mtoto wake.

Ikabidi wafanye maombi kidogo hata kama hajajua bado kinachoendelea, siunajua kila hatua dua

Sasa asubuhi kikawa ni kisanga kuwaeleza nini kimetokea maana anaona aibu alichokifanya ni ushetani kwa mtoto wa mchungaji kufanya vile.

Na wakati huo wazazi wamekazana wanataka kujua ni shida gani ilimpata kama mtoto wao. Wakati huo huo

bado amepigwa na bumbuwazi kilichotokea kule



Eeh bhana hii story ni ndefu kidogo.

Kumbuka sehemu ya kwanza tulianza kwa kumuona Nickson akija ndani ya kanisa na kuwa mtumishi mzuri sana na aliyewasaidia watu wengi ndani ya kanisa

akiwemo mchungaji mwenyewe

Lakini mwanzoni kabisa nilikuambia huyu jamaa ni mganga wa kienyeji.

Bado hatujapata majibu ya kwanini huyu mganga alijigeuza malaika na kuja kanisani? Anatafuta nini huko? Lakini pia hatujajua kanisa litamgunduaje kuwa huyo sio muumini wa kweli, bali ni wakala wa shetani

Bila shaka hili tukio lililotokea kwa Joselina lina kitu litakachozaa. 

Ni kitu gani? bado hatujajua!


Unaweza kupata mapumziko mafupi kwa ajili ya kuendelea na sehemu ya tatu ya moto huu unaitwa WAKALA WA SHETANI 



SEHEMU YA TATU


Siku moja aliyekuwa muumini wa kanisa lile alilokuwa akisali yule mganga aliyejigeuza kuwa mtumishi wa kanisa, alikuwa amesimama nje kwenye nyumba yake.

Ghafla akaja mwanamke ambaye alionekana kuwa na wasi wasi sana. Yule muumini aliitwa Onesmo


Onesmo alikuwa pia kiongozi wa kanisa kwa bahati nzuri, sasa huyo mama alipofika kwake Onesmo alimuomba kuongea naye.

Sasa kwa jinsi alivyokuwa na wasiwasi, ilibidi Onesmo afanye haraka kumkaribisha ndani.

Kama mtumishi wa kanisa hayo mambo ni ya kawaida sanaa


Hivyo aliketi na kuanza kumsikiliza.

Kumbe yule mama naye alikuwa ni muumini wa kanisa hilo japo yeye alikuwa ndio wale wanahudhuria

jumapili moja kwa mwezi, japo alifahamu na kushiriki mambo yote ya msingi ya kanisa.

Alianza kumueleza Onesmo kuwa rafiki yake ambaye sio mtu wa Kanisani, alikuwa akimshauri kuwa kwa Sababu

biashara zao zinaenda vibaya kila kukicha ni bora watafute namna vinginevyo umaskini utawaua. 

Rafiki yake akawa anamwambia kuwa “umekuwa mtu wa maombi na kanisani lakini wapi maisha yetu ndo yanazidi kuwa magumu kifedha. Lakini angalia akina mama Sethi na Hamisa walivyo

siku hizi, utadhani hatukuanza nao maisha.

Mimi nimeongea nao na zaidi sana nimeongea na mama Sethi wamenielekeza mahali. Kiufupi ni kwa mganga anaitwa Tulimba, huyo

unaambiwa ni kiboko yao. Dada tuchangamke, umaskini ni mbaya kama

Kifo”



Sasa huyo mama akaendelea kumueleza Onesmo

kuwa walibishana kwa muda na rafiki yake lakini

mwisho wa siku na yeye maisha hayo yalikuwa yameshamchosha akaona ni kweli wacha wakatafute solution

Basi mama sethi akawapa taarifa zote za kufika kwa huyo mganga Tulimba, alikuwa anakaa mkoa wa jirani

na wilaya ya ndani kabisaa. Lakini Kwa Sababu walikuwa na shida ilibidi waivumilie hiyo safari ndefu mpaka walipofika wilaya hiyo na kijiji hicho ambacho kiuhalisia hakikuwa kama vijiji vingine.

Kilikuwa kimechangamka sana Kama mjini hivii, na watu wa kule atleast

walikuwa na maisha. Imagine kijiji kilikuwa na guest houses ambapo walifikia mojawapo, ndo ujue kilikuwa

kimeendelea sana.

walienda moja kwa moja mpaka kwa mganga huyo. Walifika na kukuta wanawake wawili wakiwa na

watoto wa humo ndani. Na nyumba ilikuwa ni nzuri sio yale maisha ya waganga ambayo huwa tunawaona

kwenye movie.



Basi wakajitambulisha na walikuta pia kuna wageni kadhaa ambao walikuwa

Wamekuja kwa ajili ya shida zao kama wao. Wale wanawake wakajitambulisha kwao kuwa wao ndo wake wa mganga huyo.

Na watoto watakao waona pale ndiyo familia ya mganga huyo.

Wakaambiwa mganga ametoka lakini atakuja sio muda mrefu, na kwamba kwa bahati nzuri wamekuja

siku bayo sio ya weekend kwani ndizo siku ambazo huwa hayupo kabisaa.

Sasa baada ya muda fulani wakaambiwa mganga yupo katika chumba chake cha uaguzi na waanze

kuingia mmoja mmoja kulingana na wa kwanza kufika.

Maelezo hayo yalitolewa na aliyekuwa msaidizi wa huyo mganga

Waliingia wengine mpaka ilipofika zamu ya huyo mama kuingia pamoja na rafiki yake.



Alijiskia kuzimia pale alipoinua macho yake na kuona mzee Dickson ndiye huyo mganga.

Kwa haraka haraka anaweza kuhisi kamfananisha lakini Kumbe alikuwa Dickson kweli (tulimuona tangu

sehemu ya kwanza) maana hata na yeye alishangaa kumuona

huyo mama. 

Wakashangaana wote. Kwa mshtuko alioupata huyo mama alishindwa hata

kukimbia. Sasa rafiki yake huyo mama hakuwa anamjua huyo Dickson hivyo akaanza kuwashangaa wao.

Dickson akamwambia huyo mama, “mimi ndio mganga Tulimba hakuna mtu anaitwa Dickson, nilikuja kwa ajili

ya kazi yangu huko kanisani na lazima niimalize kabla wote hamjajua ukweli kuwa mm wala sio mtumishi wa

Mungu kama mnavyofikiria

Na Kwa Sababu wewe umeujua ukweli mapema utabaki hapa chakula cha wakuu wangu. Kama hawatakupenda, utarudi baada ya kazi yangu kuisha.

Akamgeukia rafiki yake huyo mama, akamwambia, hii inakuhusu na wewe kwa Sababu mko wote, siwezi

kukuachilia.” 



Huyo mama akaendelea kumsimulia Onesmo kuwa baada ya hapo ghafla walijikuta wapo kwenye chumba

kimejaa giza tupu. Halafu wakawa wanasikia sauti za watu ambao wananguruma tu wala hawawezi

kuongea. Kwa hiyo peke yao ndani ndo walikuwa na uwezo wa kuongea. Waliogopa mnoo. Lakini wakawa hawana cha kufanya.

Walikaa humo kwa muda ambao hawajui ulikuwa ni kiasi gani.

Mara ghafla huyo mganga akaja humo ndani na kumwambia rafiki yake huyo mama kuwa “wewe wakuu wamekutaka kabla ya mwenzio” na mara akaondoka tena.



Walijiskia kufa

Mama alimwambia Onesmo, “sijui kilitokea nini lakini tulishangaa ghafla anakuja mtoto ambaye tulimuona

kuwa ni mwanafamilia mule. Alifungua mlango na kutupaka dawa fulani hivii machoni na miguuni. Halafu akasema kimbieni msijifute macho wala miguu

vinginevyo mtaonekana. 

Hatukuamini macho yetu.



Tulikimbia kama tumefungwa engine miguuni mpaka kituo cha magari tukapanda gari ambalo tulikuwa hatujui hata tunaenda wapi. Tulishushwa

mbele sanaa huko Kwa Sababu hatukuwa na nauli.

Tuliomba lift gari ya mizigo iliyokuwa inakuja huku na kwa sababu tulikuwa wa kike tulikubaliwa.

Na sasa nimeogopa hata kufika kwangu nimekuja moja kwa moja kwako. 

Rafiki yangu yeye amekimbilia

kwa shekhe wa msikiti wake.”



Ikabidi Onesmo amchukue haraka haraka mpaka kwa mchungaj. Ile wanafika kwa mchungaj wakakuta

mchungaj na yeye yuko anasimuliwa na binti yake Kilichomtokea kama tulivyoona sehemu iliyopita (ya pili)



Onesmo akamuomba tena huyo mama amsimulie mchungaji, akamsimulia, mchungaji alilowa mwili mzima kwa jasho maana mshtuko ulikuwa ni mkubwa sanaaa. Akawaelezea na yeye ya binti yake.

Kumbe sababu ya mauzauza yale kwa Joselina, huyo mtu sio mtu wa kawaida. Na kumbe ndio maana alikuwa hana familia na wala hataki. Familia yake

ilikuwepo na ndo ipo huko nyumbani ugangani. Na ndio maana kumbe katikati ya wiki alikuwa haonekani

anasema yupo kwenye biashara zake.



Sehemu ya mwisho iliyobaki tutaona sababu kubwa ya huyo mganga kujigeuza mtumishi mzuri mpaka kuwa kiongozi wa kanisa hilo, nia yake ilikuwa ni nini.

Tutaona pia kwanini yule mtoto aliamua kuwasaidia wale akina mama.

Na mwisho wa huyo mganga

aliyejigeuza malaika tutauona


Unaweza kupata mapumziko mafupi sanaa kwa ajili ya kuimalizia shughuli hii hatari sanaaa.



SEHEMU YA NNE 

(The Last Episode)


Mganga anakuja kutoka alipokuwa. Anakuja na hasira kali sanaa. Anafika na kumchukua mke wake mkubwa, anampiga vibaya sanaa. Mke wake

mwingine jambo hilo linamchukiza sanaaa, anaamua kuingilia kati kumsaidia mke mwenza. Mganga

anawaunganisha wote.



Anawatembezea kichapo kibaya bila huruma.

Kwanini yote hayo? Nini kilitokea?

Kumbe huyo mke mkubwa wa mganga ndiye aliyemtuma mwanae awatoe kule kifungoni wale wanawake wawili tuliowaona katika sehemu iliyopita.

Mashetani yake yule mganga yalimweleza alichokifanya mkewe



Huyo mke wake na mganga alikuwa amechoshwa na ukatili wa kishetani aliokuwa akiufanya huyo mganga. 

Zaidi sana alichukia alivyokuwa akiona wanawake wenzie wanavyotendewa ukatili na huyo mganga, ambaye alijifanya anasaidia watu kumbe kwa nyuma ndiye muuaji mkubwa

Na wake zake walikuwa wakiyajua yote. Hata wale wanawake wawili alipowakamata huyo mganga, mke

wake aliamua liwalo na liwe lakini atatumia uchawi huo huo wa huyo mganga kuwatorosha, maana kwa

kiasi fulani alikuwa anajua kuutumia kwani amekaa na huyo mganga kwa muda mrefu.



Mganga aliwafungia wake zake wote wawili kwenye gereza lake la kishetani ambalo mtu wa kawaida akifika pale haoni kitu.

Aliwaweka humo na akawaambia atawafanyia kile ambacho huwa anawafanyia watu wote wanaoingizwa

humo.


Sasa, ndugu msomaji kuna kitu cha msingi hapa naomba ukisome kwa umakini sana.



Katika mkutano mkuu wa wachawi ambao ulifanyika mara ya mwisho, huyo mganga alipaswa kupewa mamlaka kubwa katika state yao ya kichawi, lakini mkuu wao kabisaa alidai bado kuna nguvu inampungukia kubeba

Nafasi hiyo.



Hivyo anahitaji kutoa kafara kubwa sana yenye nguvu sawa na nguvu anayohitaji.

Na kafara hiyo inapaswa kuwa ya kumtoa mtu aliye mtumishi wa Mungu

ambaye ana matokeo (impacts) makubwa katika utumishi wake.

Sasa mkuu wao akamwambia huyo mganga, kuwa

“Kwa kutumia nguvu zetu za kichawi, huwezi kumpata yeyote wala kumuua, wale watu wana nguvu sanaa,

unaweza kufa wewe. Hivyo unachokihitaji ni kutumia udanganyifu, yaani mfanye yeye mwenyewe ajimalize

bila kujijua, au ajikabidhi kwako bila kujijua. Kwa hiyo nenda katika kanisa X tumia akili yako yote, nguvu na ujuzi niliokupa miaka yote kumnasa

mchungaji huyo awe kafara yetu”



Ulikuwa ni mtihani mkubwa sana kwa mganga huyo kwa sababu anafahamu jinsi ambavyo wenzake wengi

wamekufa katika kupambana kuwaangusha watumishi wa Mungu Lakini hakuwa na namna

Kwa hiyo akapanga kwenda kwenye kanisa hilo na kufanya kila atakaloweza apate kuaminika katika hilo kanisa kama ambavyo tuliona sehemu ya kwanza jinsi ambavyo alisaidia watu sanaa, akamsaidia mchungaji

sanaa katika mambo yote ya kifedha

Na akahakikisha anakuwa mstari wa mbele katika kil jambo la utumishi, lengo ni ili atakapoaminika aanze

taratibu taratibu kuwaletea mambo ya ibada ya kishetani bila wao kujua maana wanamuamini.

Kwa hiyo akapanga kuingiza mambo taratibu na wao kwa sababu wanamuamini ni mtumishi mzuri , hata mchungaji mwenyewe anamkubali basi

watakuwa wanafanya wakijua ni mambo mema kutoka kwa mtumishi na mwisho wa siku kanisa lipoteze nguvu yake, na hapo ndipo atakapomchukua

mchungaji na wengine atakaowataka kirahisi zaidi



Huo ndio mpango uliomleta katika hilo Kanisa na hiyo ndiyo sababu ya yeye kujifanya mtumishi wa Mungu

mpaka wakamuamini na kumbe ni mchawi mkubwa hapana mfano.

Mambo haya waliyagundua mchungaji na Onesmo pamoja na yule mama na Joselina mtoto wa mchungaji wakati wakiomba baada ya kuonyeshwa katika maono.

 


Walijiskia aibu sana na kuumia mno kwa ajili ya jambo hilo

Hivyo waliona bora waende kuomba katika nyumba ile ya huyo mganga au ukipenda muite mtumishi feki

Nickson

Wakaona liwalo na liwe hata kama atakuja na kuwaitia mwizi sawa tu.



Hivyo walienda wakawaita na waumini wengine.

Wakawaeleza kinachoendelea, waumini butwaa waliyopigwa nayo, kila mmoja ana historia yake.

Hivyo walienda mpaka kwake, na kwa vile hakuwepo maana ameshagundulika hawezi kuja tena, Joselina aliyekuwa amechongesha ufunguo (tuliona sehemu Ya kwanza)

Aliwafungulia mlango wakaingia na kuanza kuomba.

Waliomba muda mrefu sanaaa na kwa bidii kubwa



Kule kwa mganga walikokuwa wamefungiwa wake

zake wawili mara walishangaa wanaona kile chumba

walichokuwa ni kimepotea. Na wao wako nje. Halafu

ile misukule haionekani.



Kwa mtu wa kawaida alikuwa anaona kila kitu kiko vile vile lakini kwa hawa ambao ndo walikuwa wefungiwa

chumba hicho cha kichawi ndo wakawa wanashangaa

Mara ghafla akaja yule aliyekuwa msaidizi wa mganga akaja analia anasema hana nguvu tena wala chochote (nguvu za kichawi)

Akasema najiskia kabisa sina kitu ni kama binadamu

wa kawaida. Lakini kibaya zaidi mzee kule tulipokuwa naye kwenye jiwe letu la kazi amepiga kelele nyingi na

kuanguka, hajainuka tena.

Wake zake na mganga wakaenda huko mliman anakotengenezea dawa zake wakakuta anatoa povu

Na huo ndio ulikuwa mwisho wa huyo mganga.

Wale wa kanisani kue waliomba mpaka wakachoka baadaye

wakafunga maombi yao na kurudi nyumbani kila

mmoja huku wakijutia mioyo yao kwa jinsi huyu

mganga aliwachezea akili na kuwaletea udanganyifu.


Baada ya kutokumuona kanisani wala mjini kwa muda, na wale akina mama hakuna kitu kiliwatokea tena wakajua kazi imeshaisha na Mungu kashafanya kazi yake.

Na baadaye kumbe kuna muumini alijitoa ufahamu akaenda huko kulipokuwa nyumbani kwa huyo

mganga huko kijijini

Alifika akazikuta habari za kufa kwa mganga huyo.

Akarudi nyumbani na kuwapasha habari.

Wakamtukuza Mungu maana ilikuwa sawa na ile methali ya ‘mchimba shimo atatumbukia Mwenyewe’



Sina cha ziada kwenye stori hii najua imekusisimua

sana, ume enjoy sana na kujifunza sana


MWISHO 


Unaweza kutupata sehemu hizi hapa pia 👇👇


Whatsap: https://wa.me/255747671795

Twitter: https://twitter.com/bayona_stories

Instagram: https://www.instagram.com/bayona_stories/

Tiktok: https://www.tiktok.com/@bayona_stories

YouTube: https://www.youtube.com/@Bayona_stories

Facebook page: https://www.facebook.com/profile.php?id=100092534499817