Tanzania wenyeji wa Maadhimisho ya Siku ya Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika.

 


Katika ukurasa wake wa Twitter, msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania ameripoti;

Maadhimisho yatafanyika Jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha, ambapo yanatarajiwa kufunguliwa tarehe 09 Julai, 2023 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi na yatafikia kilele tarehe 11 Julai, 2023 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan