Ujue ugonjwa wa BAWASILI

 UGONJWA WA BAWASIRI

Bawasiri ni Tatizo Linalotokana na Kuathirika Kwa Mishipa ya Damu(veins)  Ndani na Nje ya Sehemu ya Haja Kubwa na Wakati Mwingine mishipa Hiyo Huweza Kupasuka na Kuvuja Damu Kwenye Njia ya Haja Kubwa na Kusababisha Maumivu


pamoja na Kutoka Kinyama au Uvimbe Nje ya Mfereji wa Haja Kubwa na Kuna Uwezekano Mgonjwa Akawa na Aina zote Mbili Bawasiri ya Ndani na Nje au Kupata Bawasiri ya Ndani Pekee 

AINA ZA BAWASIRI (Haemorrhoid)

Kuna Aina Kuu Mbili za Bawasiri ambazo ni 

1. Bawasiri ya Ndani (Internal Haemorrhoid)

2. Bawasiri ya Nje (External Haemorrhoid)

BAWASIRI YA NDANI (Internal Haemorrhoid)

Ni Aina ya Bawasiri Ambayo Hutokea Ndani ya Mfereji wa Haja Kubwa Huwa Haina Maumivu na Watu Wengi Huwa Hawatambui Kama Wana Tatizo

Aina Hii Hutokana kwa Kuvimba na Kuharibika kwa Mishipa ya Ateri za Ndani ya Mfereji wa Haja kubwa

BAWASIRI YA NDANI- Hugundulika au Mgonjwa Hutambua ana Tatizo Kwa Kuona Kinyesi Kilichoambatana na Damu pia Bawasiri ya Ndani Hutoka Nje..

AINA HII IMEGAWANYIKA KWENYE MADARAJA  MANNE

Daraja la Kwanza - Haitoki mahali pake Panapohusika au Sehemu yake ya Kawaida

Daraja la Pili- Bawasiri Hii Hutokea wakati wa Kujisaidia Haja Kubwa na Kurudi Yenyewe Baada ya tukio

Daraja la Tatu- Bawasiri Hii Hutokea wakati wa Kujisaidia Haja Kubwa na Mtu Huweza Kuirudishia Ndani Mwenyewe 

Daraja la Nne- Bawasiri Hii Hutokea na ni Ngumu Kuirudisha

BAWASIRI YA NJE

Aina Hii Hutokea Kwenye Eneo la Mwisho Kabisa la Mfereji wa Haja Kubwa na Kuambatana na Maumivu Makali na Kuwashwa kwa Ngozi Katika Eneo la Tundu Hilo Pia Husababisha Mishipa ya Damu (Vein) Kupasuka na Damu Huganda na Kusababisha Aina Nyingine ya Bawasiri 

Aina Nyingine Hiyo Kitaalamu Tunaiita (Thrombosed hemorrhoid)

Chanzo Cha Tatizo Hili

Bawasiri kwa Kiasi Kikubwa hutokana na mgandamizo unaosababishwa presha inayotumika,Mara Nyingi wakati wa Kutoa haja kubwa Hasa Pale Unapojikazana hupelekea Mishipa Inayozunguka Sehemu ya Haja Kubwa Kuvutika na Kupelekea Kuvimba,Mishipa Iliyovimba kwa Maana ya Bawasiri (Haemorrhoid) Huweza Kuendelea Kukua Katika Sehemu Hiyo Ya Kutolea Haja Kubwa Hivyo Tatizo Hilo Huwapata Hasa Watu Wenye Matatizo Kwenye Mfumo wa Mmeng'enyo wa Chakula

Mfano Watu Wanaopata Choo Kigumu,Kujaa Gesi Tumboni,na Kukosa Choo.

Sababu Zingine Zinazopeleka Msukumo Huo Uongezeke ni Pamoja na 

MIMBA

Mimba Hupelekea Kupata Bawasiri Kutoka na Mtoto Aliyetumboni Kugandamiza Tumbo la Chakula na Kuleta Athari Kwenye Utoaji wa Haja Kubwa

Bawasiri Inayosababishwa na Mimba Hupotea Baada ya 

Mama Kujifungua

Kuharisha Kwa muda Mrefu

Kitambi au Uzito Mkubwa

Kufanya Mapenzi Kinyume na Maumbile (Anal sex)

Matumizi ya Vyoo vya Kukaa Kwa Mda Mrefu

Mwili Kushindwa Kutengeneza Nishati ya Kutosha Kusukuma Uchafu Kwenye Tumbo

Dalili za Bawasiri (Haemorrhoid)

Unawezaje Kutambua Kuwa una Tatizo Hilo?

Wakati Wingine Bawasiri Inaweza Kutokea na Baada Ya Mda Mfupi Kupotea bila Dalili Yoyote 

Dalili Ambayo Wagonjwa Wengi wa Tatizo Hili Huipata ni Kutokwa na Damu Inayoweza Kuonekana Kwenye Kinyesi Au Toilet Paper Wakati wa Kujisafisha  Hasa Kwa Bawasiri ya Ndani na Uonapo Dalili Hizi ni Wazi Utakuwa na Tatizo Bawasiri  lakini Kama Utakuwa na Bawasiri ya Nje

Unaweza Kupata Kama Kiashiria cha Uvimbe Chekundu Kilichojaa Damu Pembeni ya Haja Kubwa.

Ngozi Kuwasha Katika Eneo la Tundu la Haja Kubwa

Kupata Maumivu Makali Wakati wa kujisaidia

Kujitokeza Kwa Kinyama Maeneo ya Tundu la Haja Kubwa

Kinyesi Kuwa na Damu na Kunuka Harufu Mbaya Huambatana na Maumivu Makali wakati wa Kutoa Haja Kubwa.

Uonapo Dalili Hizo Kimbia Haraka Hospital Kwa msaada Zaidi

NB: Siyo Kila Damu Inayovuja Kwenye Tundu la Haja kubwa ni Bawasiri.

Utazuia Vipi Tatizo Hili Lisikupate au Lisijirudie Kama Ushawai Kupata Matibabu?

Jitahidi Kupata Maji ya Kutosha Kila Siku Kiashiria cha Kuwa Mwili Hauna Maji ya Kutosha ni Kuona Mkojo Ukiwa na Rangi ya Njano Iliyokolea,Utumiaji wa Maji ya Kutosha Husaidia Kulainisha choo

Kuwa na Tabia ya Kutumia Machungwa,Malimao,Kabeji Nyekundu, Maharage ya Soya na Chai yenye majani Meusi.Huwa Yana Kirutubisho Kinachoitwa Flavonoids  Ambacho ni Kiungo Muhimu Sana Katika Ulinzi na Ustawi wa Mishipa ya Damu ya veini  Maana Mishipa Hiyo ndo Hupata Shida

Kula Vyakula Vyenye Asili ya Kambakamba,Tumia Mboga za Majani Kwa Wingi,Tumia Nafaka zisizokobolewa Husaidia Sana Kinyesi Kuongezeka na Kurahisisha Utolewaji Wake

Unapojisikia Kupata Haja  Hakikisha Unaenda Mara Moja Kujisaidia Kujichelewesha Kunaweza Kusababisha Upate choo kigumu

Usikae Muda mrefu Chooni Ukijisaidia Hii Inaongeza Presha Kwenye Eneo la Chini la Mishipa ya Damu na Kukuweka Kwenye Hatari ya Tatizo

Usitumie Nguvu Kubwa Kujikamua Kutoa Haja Kubwa,Tumia Misuli ya Tumbo 

Pata Choo Kwa Kuchuchumaa Kama Ilivyo Kawaida Matumizi ya Vyoo Vya Kukaa ni Moja ya Vihatarishi Vya Kupata Bawasiri Kutokana na Kwamba Unapojisaidia Uhitaji utumie nguvu kubwa Kujikamua

Ushauri Kwa Wagonjwa Kabla ya Kufika Hospital Kupata Matibabu.

Usitumie Nguvu Kubwa Kujisafisha Baada ya Kupata Haja Hii Huwa Inasababisha Ngozi Kuwa Laini na Kuvimba

Jisafishe Taratibu kwa Kutumia Maji Safi Bila Sabuni 

Chukua Beseni Weka Maji Yenye Uvuguvugu,Weka Kiasi Kidogo cha Dettol ya Maji na Chumvi Kiasi Kidgo Kaa Kwenye Hayo Maji Kwa Mda wa Dakika 15 hadi 30 fanya kila siku asubui na Jioni Kwa Matokeo Mazuri kitendo Hiki Kitaalamu Tunaita ( Sitz Bath)

Chukua Mmea wa Alovera Usafishe baada ya Kuusafisha Kinga Yale Maji Yake Kwenye Chombo Kisafi Baada ya Hapo Anza  Kupaka Mahali pa Kutolea Haja Kubwa Fanya zoezi Hilo Asubui na Jioni Kwa Mda Wa Wiki Mbili Mabadiliko Utayaona Au Unaweza Kuuchukua Mmea Huo na Kuuloweka Kwenye Maji yenye Mchnaganyiko wa Alovera  na Upake Taratibu Mahali pa Haja kubwa

Madhara Ya Tatizo Hili

Kupata Upungufu wa Damu 

Kupata Tatizo laa Kutoweza Kuhimili Haja Kubwa

Upungufu wa hamu ya Tendo la ndoa kwa Mwanaume na mwanamke

 Kuathiri saikorojia

Maumivu Makali

Kukosa Mood ya Kufanya Kazi

Vipimo na Uchunguzi

Vipimo vya Ugonjwa wa Bawasiri Hufanywa Baada ya  Historia ya Mgonjwa.

UCHUNGUZI kwa njia ya macho, kwa mgonjwa mwenye Bawasiri ya nje Dr hunchunguza mgonjwa au mteja kwa kumuangalia Sehemu yake ya Kutolea haja kubwa

Lakini kwa Bawasiri ya Ndani,huwa laini sana inaweza Kuchunguzwa kwa kipimo cha Digital rectal 

Daktari Hufanya Uchunguzi wa Utumbo Mkubwa Kwa Kutumia Kipimo cha Anoscope, proctoscope na sigmoidoscope 

Uchunguzi wa Choo Kikubwa,Mgonjwa Ataleta samplo ya Choo Kikubwa (Kinyesi Chake) na  Mtaalamu Ataangalia Kama Kina Damu,Kama Itaonekana kuna Damu Itaashiria Kuwa mgonjwa ana Bawasiri

Kipimo cha Digital Rectal au (PR)

Kipimo Hiki Daktari Atavaa Gloves na Kupakaa Kirainishi Maalumu au Mafuta  Kwenye Kidole Chake Kimoja na kisha Ataanza Kumchunguza Mgonjwa Sehemu ya Kutolea Haja Kubwa

MATIBABU💉

Matibabu ya Bawasiri Yamegawanyika Katika Sehemu Mbili na Hutegemeana na Aina ya Bawasiri

Tiba ya Upasuaji Mdgo Ambayo Hufanywa Hospital Kwa Kukikata Kinyama au Bawasiri na Mgonjwa Kuendelea na Lishe ya vyakula Lakini Tiba Hii sio Bora Zaidi Kwa Sababu Baada Ya Muda Bawasiri Hujirudia Hivyo Zingatia Ushauri Niliokupatia hapo juu Na Hii Hali Haitojirudia

TIBA nyingine Ambayo Hutolewa Hospital ni Vidonge Baada ya Kinyama Kukatwa 


AHSANTENI SANA

Imeandikwa na;

Dr. Festo Jacob Malunde

Mawasiliano: +255742846792