Twitter imepanga kufocus na Video, watengeneza maudhui na biashara katika mtandao huo

 


Twitter inapanga ku ‘focus’ kwenye ‘partnership’ katika video, waundaji (content creator) na biashara ili kufufua biashara ya kampuni ya mtandao huo zaidi ya utangazaji wa kidijitali, kulingana na wasilisho la mwekezaji na mmiliki Elon Musk na Mtendaji Mkuu mpya Linda Yaccarino ambalo lilitolewa na Reuters.

Yaccarino, ambaye alianza kama Mkurugenzi Mtendaji mnamo Juni 5, aliwaambia wawekezaji wa Twitter siku ya Alhamisi kwamba kampuni hiyo iko katika mazungumzo ya mapema na watu wa kisiasa na burudani, huduma za malipo na wachapishaji wa habari na vyombo vya habari kuhusu ushirikiano utakao wanufaisha, kilisema chanzo kinachofahamu suala hilo, ambacho kilikuwa sehemu ya wito huo katika mkutano huo uliofanyika.

Uwasilishaji huo ulikuwa mara ya kwanza kwa Yaccarino kuhutubia wawekezaji wa kampuni hiyo, chanzo kilisema.

Baada ya Musk kupata Twitter mnamo Oktoba, kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii ilikabiliwa na machafuko ya miezi kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuachishwa kazi kwa maelfu ya wafanyakazi, ukosoaji juu ya udhibiti uliolegea wa maudhui, na kuhama kwa watangazaji (advertisers) wengi ambao hawakutaka matangazo yao yaonekane karibu na maudhui yasiyofaa.

Musk kumuajiri Yaccarino, mtendaji mkuu wa utangazaji (advertising) wa muda mrefu ambaye aliboresha uuzaji wa matangazo ya kisasa katika kampuni ya burudani na habari inayomilikiwa na Comcast NBCUniversal, ilikuwa ishara kwamba matangazo ya kidijitali yalibaki kuwa kipaumbele kwa Twitter.

Baadhi ya makampuni ya ununuzi wa matangazo yalikuwa yamependekeza wateja wao kusitisha matumizi ya matangazo kwenye Twitter baada ya Musk kuchukua madaraka.  Mapendekezo hayo yamebatilishwa na hakuna kampuni kubwa inayoshikilia utangazaji inayopendekeza kusitisha kwa sasa, kulingana na slide iliyoonyeshwa wakati wa wasilisho.

Brands maarufu zikiwemo Warner Bros, Mondelez, McDonald's na Walmart zimeanza tena kutangaza kwenye Twitter baada ya kusitisha kwa mara ya kwanza, slide ilisema.

Yaccarino aliwaambia wawekezaji kwamba matumizi ya matangazo katika category kadhaa za watangazaji sasa yamepanda kwa angalau 40% mwaka baada ya mwaka, ikijumuisha afya, bidhaa zilizowekwa kwenye vifurushi vya watumiaji na huduma za kifedha, chanzo kilisema.

Chini ya Musk, Twitter ilibadilisha jina lake la biashara kuwa X Corp., ikionyesha maono ya bilionea huyo kuunda "app bora," kama WeChat ya Uchina, ambayo alisema itajumuisha malipo ya kidijitali na huduma zingine.

Twitter inatuma ombi la "leseni za kutuma pesa" katika majimbo yote 50 ya U.S., kulingana na slide kutoka kwenye wasilisho.

Kampuni pia imezingatia kukuza maudhui ya video kwenye app.  Video ya wima (vertical video) sasa inachukua zaidi ya 10% ya muda unaotumiwa kwenye Twitter, slaidi nyingine ilisema.

Mtangazaji wa zamani wa Fox News Tucker Carlson alizindua kipindi kipya mapema mwezi huu kwenye jukwaa kinachoitwa "Tucker kwenye Twitter."

Twitter inafikiria kwamba inaweza kuuza matangazo na ufadhili (sponsorship) pamoja na video kutoka kwa Carlson na waundaji wengine wa maudhui, chanzo kilisema.

Yaccarino pia amewaambia wenzake katika siku za hivi karibuni kwamba Musk ameonyesha kuunga mkono sana mawazo yake na uhusiano wa kufanya kazi ulikuwa na mwanzo mzuri, chanzo kiliongeza.