SIMULIZI: PENZI LA CLARA NA CHRISTIAN (Sehemu ya 1)

 


Christian na Clara walimaliza shule moja ya ‘advance’ ambayo ilikuwa ni mixture, yaani ya wavulana na wasichana. Walipendana na kuingia kwenye mahusiano tangu wakiwa huko shule na mpaka sasa wameoana tayari.


Kwa upande wa Christian uwezo wake darasani haukuwa mzuri sana na wala shule hakuipenda. Alipata ‘division IV’ na hakuweza kuendelea na chuo

kikuu na wala hakutaka mambo ya kwenda diploma kwa cheti cha sekondari (o-level) kwani elimu haikuwa

fungu alilolichagua kabisa. Clara yeye alipata division two na akaenda chuo. Hilo wala halikuharibu chochote kwenye mapenzi yao yaliyokuwa ya dhati sanaa.


Christian alimuamini sana Clara na wala hakuwa na wasiwasi naye huko chuoni. Clara naye alikuwa mwaminifu kabisaa kwa mpenzi wake. Watu wengi kule chuoni walikuwa wakishindwa kuelewa ni kwanini Clara hataki kuwa na mtu pamoja na kuwa wanaume wengi chuo walikuwa wakimfuata. Baadhi walifahamu kuwa ana mtu ambaye hayupo hapo chuoni japo walishindwa kumuelewa anaweza vipi kuhimili mikiki mikiki ya vishawishi anavyopata hasa anapoona marafiki zake wakila maisha na watu wao wa chuo. 


Yeye wala hakujali hayo, alijua nani anampenda na hawezi ingia kwenye mtego wowote wa kumsaliti mpenzi wake kwani hana sababu ya kufanya hivo. Kwa upande wa Christian wengi walikuwa wakimueleza maisha ya wadada wanapokuwa chuo na kumuonya asijaribu kutafuta maumivu ambayo yatamtesa sana baadaye, ni bora atafute tu mtu ambaye yuko naye karibu ambaye anaona kila kitu chake na sio kuweka matumaini kwa mtu

Ambaye vishawishi ni kila mahali na hata akikusaliti hautajua. Kuna wakati atakuambia yuko ‘discussion’ na

wakati kalala kwa mwanaume mwingine na hutajua na ukijua huna kitu utafanya. 


Walimshauri wenye nia mbaya na wasio na nia mbaya wote hakuna ambaye

alikuwa upande wa yeye Kuendelea kuwa na Clara kama mwanamke ambaye ana mipango naye. 


Moyo wa Christian ulikuwa umeshapenda na ukaamua kuamini, yaliyobaki yote yalikuwa ni “kumpigia mbuzi Gitaa”. 


‘Misunderstandings’ kati yao zilikuwa zinatokea kama binadamu ambao sio wakamilifu  hilo ni jambo la kawaida na wala halikuwafanya kupoteza nia ya mapenzi  kati yao.


Naam, Clara alifanikiwa kumaliza chuo akahitimu. Kwa hiyo kile ambacho wengi waliona hakitawezekana, sasa kimewezekana. Sasa, ufaulu wake kwa ujumla ulikuwa ni mzuri na ulikuwa unamruhusu kuendelea na ‘masters’


Kusoma kilikuwa ni kitu anapenda sana tofauti na Christian ambaye hakupenda Kabisa. Japo alikuwa akimsapoti sana Clara kwenye masomo yake.

Hivyo alimwambia Christian kuwa ana nia ya kuendelea na masters. 


Halikuwa wazo baya kwa Christian

Tatizo lilikuja pale alipomuambia anataka aichukue abroad (huko nje ya nchi). Hapo ndipo Christian alichora mstari wa uvumilivu. Alilalamika na kumwambia anatafuta sababu ya

kumuacha kabisaa. Maana aliweza kumvumilia kipindi hicho cha kusoma degree kwa sababu kila alipotaka

Kumuona aliweza kumuona, lakini hapa hataweza kumuona zaidi sana anahisi watamchukua Clara wake.


Clara alijitetea sana na kumwambia kuwa kama aliweza kuwa mwaminifu kwake miaka yake mitatu aliyokuwa chuo hatashindwa kuwa mwaminifu kwa

huu mwaka mmoja na nusu wa masters anayoenda Kuchukua. Zaidi sana akamwambia yeye nia yake ni elimu ya

kutosha na yenye uhakika na kuaminiwa ambayo inapatikana katika vyuo vizuri duniani ili hata akienda

kutafuta kazi iwe rahisi kwake na aweze kupata nafasi nzuri katika kazi yake atakapokuwa ameajiriwa.


Hilo lilikuwa ni jambo ambalo Christian alilielewa vizuri tu, ila wasiwasi wake ulikuwa ni Clara kwenda huko ambapo atakuwa hawezi kumuona, kuwasiliana

kwenyewe kutakuwa ni Whatsap tu. Halafu huko abroad aliamini kabisa kuna watu ambao wana maisha ambao wanaweza kumchukua Clara kutoka kwake. Watakapoleta vishawishi na kwa

sababu Clara atajua kuwa Christian hatojua kinachoendelea ndipo atakubali tu na mwisho wa siku atamsahau na atarudi hataki tena habari zake Christian, ikiwezekana asirudi kabisa. 


Yaani kiufupi hilo jambo lilimpa sana mawazo Christian.


Sasa kibaya zaidi kilikuja pale ambapo aliamua kumwambia Clara “achana na abroad fanyia masters hapa”, halafu Clara akamwambia “siwezi maana hadi

process za scholarship nshaanza na nipo hatua za Mwisho na nilijua kabisa utakataa ndio maana nikaamua kufanya kwanza bila kukushirikisha” Sasa Clara akaamua kumgeuzia kibao Christian na kumwambia “kwanini huniamini? Au itakuwa unanicheat unafikiria unayoyafanya na mm ndio

ninafanya? Au Unafikiri hutaweza kunisubiria nikirudi ndio maana unaogopa sana mm kwenda?! Basi kama shida ipo kwako naona uniambie nijue” Hilo jambo likazua ugomvi fulani hivii, ikabidi Christian awe mpole na Akamuomba msamaha Clara,

akamwambia “basi wewe nenda mm nitakusubiria kama nilivofanya tangu mwanzo” Basi Clara akamuomba pia msamaha Christian kwa vile amekuwa mkali kwake mpaka ugomvi, wakasameheana


Clara akamuomba Christian amsaidie kumuangalia mdogo wake aliyekuwa anasoma sekondari, na yeye alikuwa hapendi shule pia kama Christian. Clara

akamuomba sana amsaidie kumfuatilia maana yeye ndiye aliyekuwa akifanya hivo hapo kabla na uzuri ni kuwa nyumbani walikuwa wanamjua chris


Maombi ya “Scholarship” yakakamilika, na akapewa “scholarship” na pia chuo alichofanya maombi ya kusoma hapo akapata akaenda kusoma France (kwa

akina Comman na Mbappe )


Ilikuwa ni baada ya miezi nane tangu Clara amefika France. Alikuwa yupo kwenye mgahawa mmoja hivi amekaa na kijana mmoja ambaye walikumbatiana na ku ‘kiss’. Na ghafla simu ya Clara aliyokuwa ameiweka

kwenye mfuko wa koti alilokuwa amelivaa Ikatoa mlio wa ujumbe kuingia. Alikuwa aweka sauti ya

juu kidogo hivo waliusikia vizuri. Sasa alivoskia mlio huo alirudi nyuma mara moja akachukua simu na kumbe ni ujumbe kutoka kwa Christian “good morning babe” Aliondoka akilia na kumuacha huyo kijana akishangaa ni nini shida.


Nina kila sababu za kukuelezea ni kwanini anaonekana amesaliti na yuko na mahusiano na mtu mwingine. Na ni kwanini anaonekana kujutia anachokifanya pale anapopokea ujumbe kutoka kwa Christian. Na je vip Christian na yeye huko hajaharibu

mambo kweli.? Hatima yao ni ipi?!

Katika sehemu ya pili tutapata majibu yote.

Usikose sehemu ya pili ya simulizi hii