Taarifa kutoka Idara ya mawasiliano ya Ikulu imesema;
Raisi Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao kuwa na hadhi ya Balozi kama ifuatavyo;
1. Dkt. Moses Kusiluka, katibu mkuu Kiongozi kuwa Balozi
2. Dkt. Salim Othaman Hamad, msaidizi wa Raisi anayeshughulikia masuala ya siasa kuwa Balozi
3. Dkt. Kasim Mohammed Khamis, msaidizi wa Raisi anayeshughulikia masuala ya hotuba kuwa Balozi
Na uteuzi huu umeanza leo Juni 13. Aidha vyeo walivyokuwa navyo vitabaki kama vilivyo na wateule hao wataapishwa Juni 16 Ikulu Chamwino Dodoma kuanzia saa nne asubuhi

FOLLOW US HERE