Kauli za Messi zilizogusa hisia za mashabiki wa Barcelona baada ya maamuzi yake ya kuamua kwenda Inter Miami Marekani

 


Baadhi ya maneno ambayo yaligusa sana hisia za watu ambao ni wapenzi wa soka, mashabiki wa mchezaji huyo mkubwa wa wakati wote katika interview yake ya usiku wa kuamkia jana ni pamoja na;

"Nilisikia kwamba [Barca] ilibidi kuuza wachezaji au kupunguza mishahara ya wachezaji na ukweli ni kwamba sikutaka kupitia hilo." Hapa alikuwa akizungumza juu ya mipango ya Barcelona kuweza ku accomodate gharama za mchezaji huyo kulingana na sheria za La Liga walitakiwa kufanya hivo ambapo ni pamoja na kuuza baadhi ya wachezaji na kuwapunguzia pia baadhi mishahara yao, lakini yeye ameona hilo halitakuwa sawa kabisa kwake.

"Barca kushinda La Liga msimu huu? Ndiyo, nilifurahi, niliifuata mwaka mzima na nilitaka Barca ishinde kama ilivyo nia ya kila shabiki wa Barcelona." Kauli hii ilionyesha sana mapenzi yake makubwa kwa club hiyo kubwa katika soka la Ulaya na dunia nzima kwa ujumla. Hili alilithibitisha zaidi pale aliposema 

"Ukweli ni kwamba nilikuwa na ofa kutoka kwa timu nyingine ya Ulaya, lakini hata sikutathmini kwa sababu Ulaya wazo langu lilikuwa ni kwenda Barcelona tu."

Kila la kheri kwake Messi katika timu yake mpya aliyoelekea Inter Miami ya huko Marekani