Balozi wa Romania nchini Kenya ambaye anadaiwa kufananisha tumbili na Waafrika wakati wa mkutano katika mji mkuu ameondolewa, kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Romania.
Dragos Viorel Tigau alikuwa katika jengo la Umoja wa Mataifa jijini Nairobi mnamo Aprili 26 wakati tumbili alipotokea kwenye dirisha la chumba cha mkutano.
Dragos Viorel Tigau anadaiwa kufananisha tumbili na Waafrika alipokuwa akihudhuria mkutano jijini Nairobi.
Wizara ya mambo ya nje ya Romania ilisema iliarifiwa kuhusu tukio hilo wiki hii pekee na 'ilianza utaratibu wa kumwita balozi wake'
Balozi wa Romania nchini Kenya ambaye anadaiwa kufananisha tumbili na Waafrika wakati wa mkutano katika mji mkuu ameondolewa, kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Romania.
Dragos Viorel Tigau alikuwa katika jengo la Umoja wa Mataifa jijini Nairobi mnamo Aprili 26 wakati tumbili alipotokea kwenye dirisha la chumba cha mkutano.
"Kundi la Afrika limejiunga nasi," Tigau alisema, kulingana na barua kutoka kwa ubalozi wa Sudan Kusini nchini Kenya iliyoonekana na shirika la habari la AFP.
"Kundi la Afrika lingependa kukemea kwa nguvu zote matamshi ya matusi, ubaguzi wa rangi na udhalilishaji," aliandika Chol Ajong'o, balozi wa Sudan Kusini nchini Kenya ambaye anaongoza wanadiplomasia wa Afrika mjini Nairobi.
Wizara ya mambo ya nje ya Romania ilisema Jumamosi kuwa ilikuwa imefahamishwa tu kuhusu tukio hilo wiki hii, na baada ya hapo "ilianza utaratibu wa kumwita balozi wake".
"Tunajutia sana hali hii na tunatoa pole kwa wale wote ambao wameathirika," iliongeza, ikisema tabia ya ubaguzi wa rangi au maoni "hayakubaliki kabisa"
Tigau "aliwasilisha msamaha wake, ikiwa ni pamoja na kwa maandishi", wizara hiyo ilisema, na kuongeza kuwa taarifa yake iliwasilishwa kwa mabalozi wa Afrika huko Bucharest mnamo Juni 9.
Wizara ya mambo ya nje ya Romania "inatumai kuwa tukio hilo halitaathiri uhusiano na nchi za bara la Afrika", taarifa hiyo iliongeza.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe 21 - wanane binafsi na 13 mtandaoni, kulingana na gazeti la Kenya The Daily Nation.
Mwanadiplomasia wa Kenya Macharia Kamau alisema kipindi hicho "kilimshtua na kumchukiza".
"Aibu kubwa inajaribu kuficha aibu hii. Hili [hali] halivumiliki na halikubaliki katika enzi yoyote, achilia (ya) karne ya 21,” aliandika kwenye Twitter.
Baadhi ya wanadiplomasia wa Afrika wametoa wito wa kuomba radhi kwa umma kutokana na matusi hayo, kulingana na gazeti la The Standard.

FOLLOW US HERE